Kocha wa muda katika timu ya Yanga, Boniface Mkwasa, amesema kitendo kilichofanywa na David Molinga cha kukasirika mara baada ya kufanyiwa mabadiliko ni utovu wa nidhamu.
Kauli hiyo imekuja mara baada ya Molinga kufanya hivyo jana walipocheza dhidi ya JKT Tanzania, mechi ambayo waliibuka na ushindi wa mabao 3-2.
Kutokana na hasira za Molinga, Mkwasa amemtaka mchezaji huyo kuacha tabia na badala yake akubali pindi inapotokea anafanyiwa mabadiliko.
Amesema mabadiliko ni sehemu ya kimbinu na hakuna sababu ya kukasirika kwani yanakuwa na malengo na huwa haimaanishi kuwa mchezaji amechoka wala hana kiwango kizuri.
WANAYANGA PATENI MAJIBU AMBAYO NI HAKI YENU KWA HAYA YAFUATAYO
ReplyDelete🔛Ningependa kuwashauri wanayanga kuulizia na kufahamu mambo yafuatayo ambayo bado yanautata....ambayo wengi hawajapata majibu yanayoridhisha na yasipopatikana yanaweza "kuchafua hali ya hewa" pale mtaa wa Twiga & Jangwani.
⛔ Kocha Mkuu & Benchi La Ufundi lililo Bora na La Kisasa
Baada ya Kuondolewa na Kuvunjiwa Mkataba Mwalimu Mwinyi Zahera na Msaidizi wake Noeli Mwandila na Benchi lote ka Ufundi...Liliundwa benchi la muda likiongozwa na Charles Boniface Mkwassa akisaidiana na Saidi Maulidi SMG.....hawa waliambiwa wanashikilia timu kwa Wiki 2 wakati ambapo Kocha wa Kudumu anatafutwa.
Ukiangalia Ligi Kuu ilivyo...na Malengo ya Klabu kuchukua ubingwa....lazima apatikane Kocha Mkuu mwenye kiwango zaidi ya Mkwassa kwani kulikuwa hakuna haja ya kumfukuza Zahera ikiwa hawakuweza kumpata mwalimu mwenye uwezo wa juu zaidi ya Mkwassa....bado ili timu ishindane kwa ubora na uimara katika kiuchezaji na timu kama Simba au Azam lazima Kocha wa Kudumu awe anatokea katika nchi zilizo na uwezo na utaalamu wa kufundisha soka zaidi ya walimu wanatokea ukanda huu wa Afrika (Mashariki, Kati, Kusini na Magharibi)
⛔ Ushauri Kuhusu Kocha
Kocha wanaotokea Serbia, Yugoslavia, Scotland, Amerika Kusini ama Ulaya Magharibi watafaa kuifundisha Yanga kwani Timu inatakiwa iimarike kiuchezaji na kifalsafa
⛔ Kuacha Visingizio Vya Ukosefu wa Pesa
Kuna dhana inayojengeka kuwa Timu haina fedha kwa hiyo tuiishie kufundishwa na wazawa ambao uwezo wao ni wa kawaida hii ni dhana potofu ambayo haina ukweli wowote. Yanga ni timu kubwa ambayo ina udhamini wa makampuni zaidi ya 4 (SportPesa, Taifa Gas, GSM, Maji ya Afya, Azam Media) pamoja na Vodacom....pili Yanga ina wanachama na mashabiki wenye uwezo mkubwa wa kifedha wanaojitolea kuilipia gharama kubwa kubwa mifano mingi ipo kudhihirisha hili kama ambavyo ilivyofanyika huko nyuma. Isitoshe, Kuendana na Ukubwa wa Jina la Yanga na msukumo unaotokana na Uwekezaji uliofanyika Simba itakuwa ni aibu kwa Yanga kutoingia kwenye mabadiliko ya kiundeshaji na kupata mwekezaji ama wawekezaji/ ambao wana uwezo kuzidi hata huyo aliyepo Simba...
⛔ Uwanja wa Kaunda na Kigamboni
Kumekuwa na kusuasua na mwendo wa kinyonga katika utekelezaji wa ukarabati na ujenzi wa uwanja wa mazoezi wa Yanga. Wapenzi na Mashabiki wanahoji hili na hasa wanapoona wenzao mtaa wa Pili wao wamekamilisha uwanja wao...ila Yanga zimebaki porojo na siasa tu....ILI LAZIMA LIISHE WANAYANGA WAMECHOKA WANATAKA VITENDO
🚫 Maswali
✔ Kwanini kuna kusuasua na kujivutavuta kuingia katika Uwekezaji na Mabadiliko katika Yanga huku kukiwa kushindwa Kamati lukuki zilizo leta mabadiliko au kufanya Vitendo vinavyoonekana?
✔ Je, Viongozi wana nia ya dhati ya kuiinua Yanga kiuchumi? Kama wanayo mbona mchakato wa mabadiliko unachelewa?
✔ Je, Kama hauchelewi na kama haurakishwi kwanini kuna kilio cha ukata wa fedha na kutaka "KUENDESHA MAMBO KIZAMANI KWA MFUMO WA KARNE YA 19 WAKATI TUPO KARNE YA 21???? Mpira ni Pesa na Matokeo mazuri na uendeshaji wa Timu kwamaana ya Benchi la Bora la Ufundi, Miundo Mbinu Bora, Kambi na Huduma za Wachezaji Bora hutokana na Uwekezaji wa Pesa....kwani Uongozi uliochaguliwa ulisema ndani ya Miezi 3 hadi 6 wataiingiza Yanga katika mabadiliko hili mbona unasuasua???
🚫 Wenu katika kutoa ushauri chanya kwa ajili ya Maendeleo ya Mpira Tanzania!
Ahsanteni
Mwalimu Mkwassa anasema anatoa mapumziko ya siku 3 kwa maoni yangu hayo mapumziko ni mengi mno....mimi nilifikiri kwakuwa wachezaji wa timu ya Taifa wamerudi wangeendelea kujumuika na wenzao ili kuanza kuelewana mfumo wa timu kupitia benchi jipya la ufundi....wachezaji wanapunguza stamina ya kucheza kwa dakika 90 pindi unapowapa mapumziko marefu...utakubaliana na mimi kuwa wengi wanakuwa wazito pindi wanapotoka kwenye break...kwa hiyo Mwalimu angeendelea kuwaunganisha kwa kuwapa mazoezi kwani na hizi mvua zinazoendelea kuna wasiwasi kuwa huko mbele timu ikashindwa kukutana na kufanya mazoezi ya pamoja....wakati ni huu kuendelea kutoa dozi mfululizo bila kupumzika pumzika...
ReplyDelete
ReplyDelete1. Kutoa CD/DVD zenye mkusanyiko wa mechi zote zilizochezwa miaka ya Nyuma ambayo iilifanya Yanga Kuchukua Ubingwa mara 27 na kufanya kuitwa mabingwa wa kihistoria ikiwemo Matukio yote yaliyofanyika kabla, wakati na baada ya Wiki ya Mwananchi iliyoadhimishwa Tanzania nzima
2. Kutoa na Kuuza Nakala ama Chapisho la Kila Wiki kwenye mahojiano na wachezaji/familia za wachezaji/wanachama/wapenzi walio ndani na nje ya nchi/wachezaji wa zamani mashabiki nguli walio serikalini, sekta ya umma, sekta binafsi kwenye taasisi za serikalini na balozi
3. Kutoa Nakala Chapisho lenye Mahojiano ya Wadhamini wa Yanga, TFF, BMT, Viongozi wa Yanga. Wawakilishi wa Matawi, Wazee wa Yanga, Benchi la Ufundi na Secretariat ya Yanga
4. GSM Kutengeneza vifaa na jezi, fulana, kofia na vifaa vinavyohusiana na hivyo (Kanga, shuka, vitambaa na benders ndogondogo) zenye Nembo ya Yanga
Ahsanteni