November 23, 2019


Mkufunzi wa Tottenham, Jose Mourinho anatafakari uwezekano wa kuvunja jaribio la AC Milan la kumsajili mshambulizi mahiri wa Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, na kumleta nyota huyo London. (Telegraph)

Kocha wa Lille Christopher Galtier amemkosoa Mourinho kwa kuwanunua maafisa wawili katika kundi lake la wakufunzi kujiunga na Spurs. (RMC Sport via Evening Standard)

Meneja wa West Ham Manuel Pellegrini anasema Mourinho sio rafiki wala adui wake . (Talksport)

''Mourinho sio rafiki wala adui yangu'' asema mkufunzi wa West Ham Manuel Pellegrini
Mkufunzi wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino ananyatiwa na Bayern Munich kushikilia wadhifa wa kocha wa kudumu. (Sky Sports)

Barcelona pia wanamtaka raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 47, ambaye aliwahi kuwa meneja wa mahasimu wao Espanyol. (Sun)

Kiungo wa kati wa Arsenal na raia wa Uruguay Lucas Torreira, 23, hajapinga uwezekano wa kuondoka klabu hiyo mwezi Januari. (Sport 860 via Mirror)

Lucas Torreira (kulia) alianza mechi tatu za Uruguay katika michuano ya kombe la dunia, ikuiw ani pamoja na mechi ya robo fainali ambayo walishindwa na Ufaransa

Mshambuliaji anasalia kuwa kipaumbele cha Manchester United mwezi Januari- na mkufunzi Ole Gunnar Solskjaer amekuwa akifanya mikutano ya kila mwezi na timu yake ya usajili katika juhudi ya kufikia orodha ya wachezaji watatu. (Evening Standard)

Winga wa Celtic raia wa Norway Mohamed Elyounoussi, 25, amedokeza kuwa Stuart Armstrong atahamia Parkhead kwa mkopo. (The Scotsman)

Sunderland huenda wakamsajili beki wa kushoto na kulia wa Uingereza Marcus Maddison,26, kwasababu Peterborough wamekataa kupunguza bei yao. (Newcastle Chronicle)

Gerard Pique aliichezea Barcelona mara 52 msimu uliopita
Mlinzi wa Uhispania Gerard Pique, 32, anasema atamaliza taaluma yake ya michezo katika klabu ya Barcelona ifikapo mwaka 2022. (Mundo Deportivo)

Mkufunzi wa Paris St-Germain, Thomas Tuchel anasema hakuridhishwa na hatua ya mshambuliaji Neymar kwenda Madrid kuhudhuria kombe la Davis. (Marca)

Ajenti wa kiungo wa kati wa Real Madrid, Gareth Bale anasema kuwa mchezaji hujaathiriwa na hatua ya mashabiki wa Los Blancos kufuatia piacha aliyopiga akiwa na bendera iliyoandikwa, 'Wales. Golf. Real Madrid. Katika usanjari huo'. (ESPN)

KUTOKA BBC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic