MKWASA AZUNGUMZIA USAJILI WA KIUNGO FUNDI KUTOKA RWANDA
Kaimu Kocha wa Yanga, Boniface Mkwasa amefunguka kuhusiana na usajili wa Haruna Niyonzima ndani ya kikosi chatimu hiyo. Imeelezwa.
Taarifa imeeleza kuwakKocha huyo ambaye amechukua nafasi ya Mwinyi Zahera kwa muda, amesema kwa sasa hawezi kuongelea zaidi juu ya usajili japo akikiri Niyonzima ni mchezaji mzuri.
“Ndio kwanza nimechukua timu, sijapata muda wa kutosha, lakini nautumia muda huo kurejesha timu kwenye morali yake, kila mchezaji Yanga ana thamani na anapaswa atimize zaidi ya jukumu lake la msingi.
“Masuala ya usajili na huyo Niyonzima uliyomtaja, kumbuka mimi ni kocha wa muda kama nitakuwa bado nimepewa nafasi ya kuendelea na kufanya usajili nitazungumzia hilo, Niyonzima ni mchezaji mzuri bado ana nafasi ya kuichezea Yanga,” alisema.
Ikumbukwe huko nyuma tayari Niyonzima mwenyewe alibainisha utayari wake kurejea kuicheza timu ya Wananchi, Yanga, ikiwa ni siku chache baada ya kukutana na mwenyekiti wa zamani wa kamati ya usajili, Bin Kleb nchini Rwanda.
siaje
ReplyDelete