MZAMBIA ATUMIWA TIKETI YANGA
Viongozi wa Yanga, juzi walimtumia tiketi ya ndege mshambuliaji wao, Mzambia Mybin Kalengo ili arejee nchini kupata matibabu ya haraka yatakayomrudisha uwanjani mapema.
Mshambuliaji huyo kinda hivi karibuni alirejea nyumbani kwao Zambia kwa ajili ya kuuguza majeraha baada ya kufanyiwa upasuaji kufuatia kuvunjika mguu akiwa kambini jijini Mwanza.
Kalengo aliumia kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Pamba FC, alifanyiwa upasuaji Hospitali ya Muhimbili jijini Dar es Salaam aliporudishwa kwa ajili ya matibabu.
Mkuu wa Kitendo cha Habari na Mawasiliano wa Yanga, Hassani Bumbuli alisema kuwa mshambuliaji huyo atarejea nchini kwa ajili ya kupatiwa matibabu na madaktari bingwa ili arejee uwanjani mapema.
“Kalengo tumemtumia tiketi ya ndege ili arejee haraka nchini kwa ajili ya kuendelea na matibabu ya karibu chini ya madaktari wa moja ya hospitali ili kuhakikisha anapona kwa haraka,” alisema Bumbuli.
0 COMMENTS:
Post a Comment