November 30, 2019


UONGOZI wa Klabu ya Yanga umedaiwa kuwa upo kwenye harakati za kutaka kumrudisha Mrundi, Amissi Tambwe kikosini hapo kwa ajili ya kuiongezea nguvu safu ya ushambuliaji ya timu hiyo.

Hatua hiyo imekuja baada ya kutovutiwa na uwezo wa baadhi ya washambuliaji wa kimataifa wa timu hiyo ambao tangu kusajiliwa kwao wamekuwa na wakati mgumu, ikiwa na maana kuwa Tambwe yupo mguu sawa kuja Dar es Salaam kwa sababu mbili kuu, moja ikiwa ni hiyo ya kusajililiwa.

Tambwe alisema kuwa juzi Jumatano alifanya mazungumzo na mmoja wa viongozi wa juu wa Yanga na kumwambia mpango huo. “Aliniambia kuwa kwa washambuliaji waliopo sasa kikosini hapo hakuna ambaye ananizidi kiwango.

“Kwa hiyo kutokana na hali hiyo ni bora wanirudishe ili niweze kuwasaidia kwani wanaamni uwezo wa kufanya hivyo ninao,” alisema Tambwe ambaye sasa ni mchezaji huru baada ya kuvunja mkataba na Klabu ya Fanja ya Oman ambayo alijiunga nayo baada ya kutoka Yanga.

Hata hivyo, alipotakiwa kumtaja kiongozi huyo, alisema: “Siwezi kumtaja kwa sasa lakini muda utakapofika nikipata ruhusa yake basi nitamtaja kiongozi huyo ila ni wa juu.”

Sababu nyingine ya kumrejesha Dar ni kuwa hadi sasa bado hajamalizana na Yanga katika suala la malipo baada ya kuvunjwa kwa mkataba wake uliopita.

Alipoulizwa Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli kuhusu ujio wa Tambwe alisema: “Sijapata taarifa hizo mezani kwangu, tunaheshimu mchango wa Tambwe, aliipa mafanikio makubwa timu yetu na kama kuna lolote tutatoa tamko rasmi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic