November 15, 2019


Nikola Kavazovic anatajwa kuwa mrithi wa Mwinyi Zahera kunako Klabu ya Yanga.

Kocha huyo ambaye ni raia wa Serbia alishawahi kufundisha vilabu vya Township Rollers ya Botswana (2017-2018), Leopards ya Kenya mwaka 2018 na Klabu ya Free State ya South Afrika msimu huu wa (2018-2019).

Kavazovic anaonekana kulijua vyema soka la Afrika kutokana na uzoefu wake wa kufundisha klabu kadhaa hapa Barani Afrika.

Klabu ya Yanga kwa sasa ipo chini ya Charles Boniface Mkwasa "Master" ambaye ameteuliwa kuwa kocha wa muda na uongozi wa klabu.

Maamuzi ya kumteua Mkwasa yalikuja mara baada ya Kamati Tendaji kufikia uamuzi wa kuvunja benchi zima la Ufundi la timu hiyo kutokana na matokeo yasiyoridhisha chini ya Zahera.

Mbali na Kavazovic, Yanga pia ilishawahi kufundishwa na makocha wa Serbia kwa miaka ya hivi karibuni kama Dusan Kondic na Kostadin Papic.

Imeandaliwa na Jose Jose

1 COMMENTS:

  1. aje tuu maana naona mzungu wa upande wa pili karibu anaaga sio mda

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic