OBREY Chirwa nyota wa Azam FC amesema kuwa hajui idadi ya mabao atakayofunga msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara.
Jana Chirwa aliiongoza Azam FC kwenye ushindi wa mabao 5-0 mbele ya Alliance FC mchezo uliochewa uwanja wa Nyamagana yeye akifunga mabao matatu na kusepa na mpira jumla huku mabao mengine yakifungwa na Idd Chilunda.
Chirwa amesema:-"Kazi yangu mimi ni kufunga suala la kujua idadi ya mabao mangapi nitafunga hilo mimi sijui, ni Mungu mwenyewe ndiye anayejua idadi ya mabao ambayo nitafunga ndani ya ligi," amesema.
Chirwa anakuwa mshambuliaji wa tatu kufunga hat trick wa kwanza alikuwa Ditram Nchimbi wa Polisi Tanzania akafuata Daruesh Saliboko wa Lipuli.
0 COMMENTS:
Post a Comment