UKIACHANA na tambo za Simba kwamba leo wataibatiza Mbeya City kwa moto Dar, takwimu tu zinawapa ushindi.
Simba ina hasira ya kupoteza mbele ya Mwadui FC kwa kufungwa bao 1-0 huku Mbeya City ikiwa imetoka suluhu na Alliance FC iliyokuwa pungufu ya wachezaji wawili.
Kitakwimu, Mbeya City imepanda daraja msimu wa 2013/14 imekutana na Simba mara 12 ambapo Simba imeshinda mara 7, Mbeya City imeshinda mara mbili na zimetoka sare tatu.
“Tunajua wapi ambapo tulikosea na tumefanyia kazi makosa yetu kazi iliyobaki ni moja tu kwa sasa kutafuta matokeo chanya,” alisema Kocha wa Simba, Patrick Aussems na kusisitiza kwamba anategemea kumaliza mchezo wa leo mapema kabisa kwa vile wachezaji wake wamepania kuwafurahisha mashabiki.
Amesema kwamba watawabatiza kwa moto kutokana na ubora wa uwanja ambao watakuwa wanateleza tu.
Juma Mwambusi, Kocha Mkuu wa Mbeya City alisema kuwa kushindwa kupata matokeo kwenye mechi zake zilizopita kumewapa darasa litakaloongeza nguvu kwao kupambana na Simba ambao hawataamini leo kwenye Uwanja wa Uhuru.
Ugumu wa mechi ya leo utatokana na rekodi hizi hapa ambazo zimewekwa na timu hizi mbili baada ya kukutana mara 12:
MABAO YA KUFUNGANA
Jumla ya mabao 28 yamefungwa ambapo Simba imefunga jumla ya mabao 18 huku Mbeya City ikishinda jumla ya mabao 10 kwenye jumla ya misimu sita ambayo wamekutana.
MECHI ILIYOLETA MABAO MENGI
Mechi mbili ndizo ambazo zilileta mabao mengi kwa Simba na Mbeya City na zote zilileta mabao manne. Ilikuwa ya msimu wa 2016/17 zilitoka sare ya mabao 2-2 Uwanja wa Sokoine na mwingine ilikuwa ni msimu wa 2017/18 Uwanja wa Taifa, Simba ilishinda mabao 3-1
MATOKEO YAO KIUJUMLA
2013/14- Simba 2-2 Mbeya City, Mbeya City 1-1 Simba. 2014/15-Simba 1-2 Mbeya City, 2-0 Simba 2015/16-Mbeya City 0-1 Simba, Mbeya City 0-2 Simba 2016/17- Mbeya City 0-2
Simba, Simba 2-2 2017/18-Mbeya 0-1 Simba, Simba 3-1 Mbeya City 2018/19- Simba 2-0 Mbeya City, Mbeya City 1-2 Simba.
WACHEZAJI WA KUCHUNGWA
Kwa upande wa Simba ni wachezaji watatu ambao ni mwiba ambao ni Mzamiru Yassin mwenye asisti tatu, Miraji Athuman mwenye mabao mawili na Meddie Kagere mwenye mabao saba na asisti mbili huku kwa upande wa Mbeya City, Peter Mapunda ametupia jumla ya mabao manne kwa sasa. MECHI IJAYO Simba vs Prisons Siku:Alhamisi ijayo
0 COMMENTS:
Post a Comment