November 3, 2019


Baada ya maneno mengi hatimaye mshambuliaji wa Yanga Mganda, Juma Balinya ameibuka na kusema kuwa hivi sasa yuko fi ti kiafya na yupo tayari kuipigania timu yake hiyo kwenye michezo ijayo ya Kombe la Shirikisho na Ligi Kuu Bara.

Yanga, kesho inatarajiwa kujitupa kwenye uwanja kucheza na Pyramids FC katika mchezo wa Kombe la Shirikisho utakaopigwa nchini Misri. Huo ni mchezo wa pili kuchezwa baada ya awa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza, Yanga kufungwa mabao 2-1.

Akizungumza na Championi Jumamosi, Balinya alisema anatamani kuona akiifanyia makubwa Yanga aliyojiunga nayo msimu huu ikiwemo kuifungia mabao.

Balinya alisema kuwa kwa kuanzia mchezo wa kesho ameahidi kuifungia na kutengeneza mabao timu yake kuanzia mchezo dhidi ya Pyramids kama akipata nafasi ya kucheza. “Hivi sasa nipo sawa kiafya, pia kiakili nafahamu mashabiki wa Yanga wanatamani kuniona nikiifanyia makubwa timu yao.

“Nimepanga kuifanyia makubwa Yanga katika michezo ijayo ukiwemo na Pyramids, ninaamini ni mchezo muhimu huu kwetu kupata ushindi. 

“Hakuna kitakachoshindikana kwangu, niwaombe Wanayanga waendelee kunipa ushirikiano ili nikifanye kile kilichonileta hapa Yanga ambacho ni kufunga na kutengeneza nafasi za kufunga mabao,” alisema Balinya.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic