November 24, 2019


TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania, Kilimanjaro Queens kesho ina kazi ya ziada kuonyesha ubora wao mbele ya Kenya kwenye fainali za michuano ya Cecafa itakayofanyika uwanja wa Chamazi kutokana na timu hiyo kuwa miongoni mwa timu ambazo zinatafuta nafasi ya kutwaa tuzo ya timu bora kwa Wanawake Afrika.

Kili Queens inakazi ya kuwanyoosha wababe hao ambao wana hasira za kuwapokonya kombe wenyeji jambo ambalo litafanya mchezo huo kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili ambazo hazijapoteza mchezo hata moja wala kufungwa kwenye mechi zao za Cecafa walizocheza.

Kili Queens ilitinga hatua ya fainali baada ya kuifunga bao 1-0 timu ya Uganda dakika za lala salama kupitia kwa nahodha Aish Mwalala dakika ya 90 akimalizia pasi ya Mwanahamis Omary 'Gaucho'.

Fainali ya kesho itawakutanisha Tanzania ambao ni wenyeji pamoja na Kenya ambao ni vinara wa kundi B.

Mbali na Kenya timu nyingine ambazo zimetinga hatua ya kuwania tuzo kwa timu bora za Wanawake Afrika ni pamoja na Cameroon, Cote d'ivoire, Nigeria, Afrika Kusini na Zambia.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic