November 23, 2019



UNAI Emery, kocha mkuu wa Arsenal amepewa mwezi mmoja kuokoa kazi yake katika kikosi hicho kwa sasa.

Mabosi wa Arsenal wanahofu kwamba, Mhisipania huyo anapoteza utamaduni wa klabu hiyo ule wa kucheza pasi nyingi tena wa soka la kuvutia ambao ulikuwa hapo kwa muda mrefu.

Gazeti la The Sun limefichua baada ya kupata taarifa kwa vyanzo vyake kuwa kocha huyo amepewa mwezi mmoja hadi ifikapo mwisho wa mwaka huu awe amebadilisha mambo.

Ana mechi tatu mfululizo akianza na Southampton, Norwich na Brighton na zote anatarajiwa kushinda.

Lakini inaelezwa kuwa Emery ana sapoti kubwa ya Mkuu wa soka Raul Sanlleh na Mkurugenzi wa ufundi Edu.

Arsenal haijapa ushindi wowote tangu wiki ya kwanza ya Oktoba kwenye Premier League na imeporomoka hadi nafasi ya sita kwenye msimamo ikimaanisha kuwa matumaini ya kushiriki Ligi ya Mabingwa Ulaya yanadidimia kila baada ya wiki.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic