November 23, 2019


IMERIPOTIWA kuwa kiungo wa Manchester United, Paul Pogba anaweza kujiunga na Juventus mwezi Januari.

Awali ilielezwa kuwa Pogba alitaka kujiunga na Real Madrid kwenye usajili uliopita dili hilo lilifeli kutokana na Madrid kukosa mkwanja uliohitajika United.

Kumekuwa na mawasiliano ya karibu kati ya nyota wa Juventus, Cristiano Ronaldo na Pogba jambo linaloongeza ushawishi wa nyota huyo kutua Juventus.

Pogba alisepa Juventus kwa kitita cha pauni milioni 89, 2016 na kujiunga na Manchester United lakini ameshindwa kuwika kwenye kikosi hicho.

Akiwa Juventus alitwaa mataji tisa, mpaka sasa amecheza mechi sita akikosa mechi 10 kutokana na majeraha ya enka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic