November 10, 2019


Mashabiki wengi wa Simba bado wanamkumbuka mshambuliaji wao, john Bocco ambaye bado majeruhi mpaka sasa.

Bocco amekuwa nje ya kikosi cha Simba kwa muda mrefu kufuatia kuumia katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC.

Wengi wao wamekuwa wakiona kama straika Mrwanda, Meddie Kagere anakosa mtu wa kusaidiana naye katika safu ya ushambuliaji kufuatia uwepo wake na Bocco kufanya vema msimu uliopita.

Hivi karibuni tulielezwa Bocco anaweza akaanza kucheza lakini inaonekana mambo hayajakaa vizuri kwake jambo ambalo linapelekea kuendelea na program maalum.

Baadhi ya mashabiki wa timu hiyo wameshauri ni vema mchezaji huyo akapelekwa hata nje ya nchi kwa watalaam ili kupata vipimo vya kina badala ya kuendelea na matibabu ya hapa nchini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic