November 10, 2019



JURGEN Klopp Meneja wa Liverpool ana kibarua kizito leo Novemba 10 uwanja wa Anfield itakapomenyana na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England Manchester City ambao ni wapinzani wao wa karibu kwa sasa ndani ya Ligi Kuu England.

Liverpool inaingia uwanjani ikiwa haijaonja ladha ya kupoteza mchezo wa ligi baada ya kucheza mechi 11 ikiwa imeshinda mechi 10 na ililazimisha sare moja ya kufungana bao 1-1 mbele ya Manchester United kwenye mchezo uliochezwa uwanja wa Old Traford huku City ikiwa imepoteza mechi mbili, sare moja na imeshinda mechi nane.

Manchester City iliyo chini ya Pep Guardiola inaingia ikiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi  wa mabao 2-1 mbele ya Southampton uliopigwa uwanja wa Etihad huku Liverpool ikipindua meza kibabe mbele ya Aston Villa ikiwa ugenini kwa ushindi wa mabao 2-1 uwanja wa Villa Park.

Liverpool ipo nafasi ya kwanza imejikusanyia jumla ya pointi 31 huku City ipo nafasi ya tatu ina jumla ya pointi 25, kwa upande wa Meneja wa Liverpool Klopp amesema kuwa anatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kupata matokeo huku Guardiola Meneja wa City amesema kuwa watafanya kazi kubwa kutafuta ushindi ugenini.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic