Imeelezwa kuwa uongozi wa klabu ya Simba umeibuka na kusema watani zao wa jadi Yanga ndiyo wamekuwa wakisambaza taarifa za Kocha Patrick Aussems kufukuzwa kazi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa katika kurasa za mitandao ya kijamii ya Radio EFM, imesema Simba wameeleza Yanga ndiyo wamekuwa wakisambaza taarifa hizo ambazo hazina ukweli.
Uongozi wa Simba umefunguka kuwa Aussems amesafiri kuelekea kwao Ubelgiji kwa ajili ya mambo ya kifamilia na anatarajiwa kurejea leo nchini.
Kocha huyo anatajwa kurejea leo ili kuendelea na majukumu ya kazi kuelekea mechi ya ligi na Ruvu Shooting.








VYURA VYURA VYURA VYURA HATA KAMA COCHA HATAKUWEPO MSIDHANI KICHAPO MTAKIEPUKA MTACHAPWA TU .SIMBA INAUWEZO WA KUAJIRI KOCHA MWINGINE SAA YEYOTE,HUYU TULIENAYE ANAWAUMIZA VICHWA SANA NA AONDOKI MPAKA KIBANO KIWAKOLEE.TULIENI SINDANO IWAINGIE VIZURI.
ReplyDeleteRadio za mbao hizo
ReplyDelete