NA SALEH ALLY
KUMEKUWA na taarifa kwamba viongozi wa Simba wangekaa kikao cha mwisho jana ili kufikia mwafaka wa suala la kocha wao mkuu, Patrick Aussems.
Simba imeamua kuachana na Aussems lakini kumekuwa na taarifa kwamba bado ni kocha
wao.
Suala hili limekuwa na mzunguko mkubwa sana ambao unatengeneza hali ya kutoelewana au kutoeleweka kati ya uongozi wa Simba, mashabiki, wanachama lakini pia vyombo vya habari hasa vile ambavyo vimekuwa vikinusa
namna mambo yanavyoendelea ndani ya klabu hiyo.
Hata kama Simba itakuwa mwisho imefikia uamuzi wa kumbakiza Aussems baada ya kikao cha jana, tayari kuna funzo ambalo tumepata na hakika litakuwa jambo sahihi pande hizo mbili, kumalizana kiroho safi na heshima kubwa.
Funzo ni kwa kuwa tumeona namna ambavyo unapofikia kuna uamuzi wa kufanya halafu uongozi ukawa unasita au kuchukua muda mrefu namna yanavyotengenezwa maneno mengi.
Maneno yamekuwa mengi hadi yanafikia kuwa kero, kila mmoja anasema lake ingawa sahihi
linatakiwa kuwa neno moja tu.
Kuwa ni anabaki au anaondoka! Hadi leo, uongozi wa Simba umeonekana hautaki kuweka jambo hilo hadharani mapema.
Inawezekana labda kuna jambo linakwamisha lakini unaona wakati huohuo hata Aussems naye anaonekana kutokuwa na furaha, hakutokea katika kikao alichoitwa na viongozi, hali inayoonyesha ule utulivu wa zamani umepotea.
Ukitaka kufuatilia sana, wakati mwingine unaweza kuumia kichwa kwa kuwa hakuna sababu kubwa sana unaweza kusema inalazimisha Aussems kuondoka.
Pamoja na hivyo, Simba wanaweza wakawa wanajua zaidi uzuri na ubaya wa kocha huyo kuliko sisi sote, mwisho unasema hivi, kufukuzwa kwa kocha si jambo geni, kikubwa ni kumaliza mambo kwa usahihi.
Usahihi ni upi? Ni kuhakikisha hili suala linafikia mwisho kwa mwafaka sahihi ambao umelenga katika misingi ya kiheshima zaidi. Nitaeleza kwa
nini.
Aussems hawezi kuondoka leo katika historia ya Simba, atabaki kwa muda mrefu sana kwa kuwa
amekuwa ni kocha aliyeipeleka robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika, “no matter what.”
Wakati Simba inafikia hatua hiyo, yeye ndiye alikuwa kiongozi wa benchi la ufundi. Sifa na
heshima hiyo ni vigumu sana kuivua kutoka kwake na ukambandika mtu mwingine.
Aussems ataendelea kubaki katika sifa hiyo kwa muda mrefu sana. Atakaa hapo akiendelea kukumbushiwa na kuzungumziwa na hii ni heshima ya Simba pia. Hili ni jambo ambalo lazima likumbukwe.
Simba ikiachana vizuri na Aussems, litakuwa jambo zuri ambalo litaijengea Simba heshima kuwa ni klabu inayothamini au kujali makocha wake waliofanya vizuri au kazi nzuri hata kama
wanaondoka.
Pamoja na kumalizana naye vizuri kwa uamuzi wa kumuondoa, lazima kumlipa haki zake na mwisho akaendelee na maisha yake wakati Simba nayo ikiendelea kupambana na yake.
Kama Aussems ataondoka kwa kelele au maneno mengi, hii itachangia kwa kiasi kikubwa kuifanya Simba ionekane ni klabu inayozungumza tu kwa maneno kuhusiana na kufikia kiwango fulani cha ukubwa lakini matendo yake siyo.
Kukua hakuwezi kuwa maneno ya mdomoni tu, badala yake ni vitendo na mwisho majibu ya vitendo vyenyewe, jambo ambalo Simba kwa kuwa ina viongozi wengi wenye uzoefu wa juu katika mchezo wa soka nchini, halitakuwa
jambo gumu.
Mchezo wa mpira ni wa aina yake, kila mmoja ana wakati wake, uwe kiongozi, kocha na hata mchezaji. Ambao wamekuwa wakibaki na timu milele katika nafasi zao bila ya kushushwa cheo au kupandishwa, bila ya kuwa wakubwa sana au wadogo, ni mashabiki tu ambao ndio wamiliki au wenye timu.
Tatizo lako Saleh ni kuwa ulilolisema ni very premature. Kikao cha kamati ya maadili kimefanya maongezi nä Aussems jana.Bodi haijakutana unataka uamuzi.Wewe ni nani unaweza kusikiliza kwamba maamuzi yatolewe haraka?Yakitolewa haraka utakurupuka na kusema maamuzi yamefanyika bila kutafakari.Wacha haraka nä kiherehere muda utasema. Gazeti lenu si mliandika Zahera ni Mali ya Simba?Sasa weledi unaozungumzia si ungeaanza na wewe na wenzako.Charity begins at home.
ReplyDeleteAusems sio kocha kuipeleka Simba next level yaani kuiwezesha Simba kubeba kombe la Africa. Hata yeye mwenyewe Ausems analijua hilo. Watanzania si watu wenye kujiamini kuwaza kutwaa vitu vikubwa siku zote ni waoga na ni wa kuridhika na hali ya kawaida ila Mwafrica kusini alieajiriwa pale Simba anaweza akaonena kichaa au nuksi lakini Simba na wanasimba wakimpa ushirikiano basi hapana shaka Simba wataingia next level tena kwa kishindo. Simba wanahitaji kocha mshindani zaidi kuliko Ausems.Kumbuka ni Ausems mwenyewe ndie alipendekeza akina kotei,Niozima na wachezaji wengine kadhaa kuwachwa ili kujenga Simba imara zaidi. Tatizo kubwa la simba na wachezaji wake hasa wale mastaa wakubwa ni kupatwa na shindikizo la mawazo baada ya kutolewa mapema klabu bingwa Africa jambo ambalo hawakulitegemea. Licha ya Simba kuonywa na wadau wengi wa soka kwa mchezo m'bovu wa kiwango cha hovyo kule Msumbiji lakini kocha wao alishindwa kufanya marekebisho yoyote na hasa ile tabia ya Ausems kukata tamaa kabisa kupata ushindi ugenini Africa na kwa hali hiyo basi siioni Simba ya kuwa mshindani wa kweli Africa chini ya Aussems
ReplyDeleteSaleh Jembe acha kiherehere na mihemuko.Kama unataka kuwa Hakimu wa hiyo kesi basi waombe Simba ukatoe hukumu maana wewe no mlalamikaji,mlalamikiwa,mtetezi na hapo halo Hakimu.Kumbuka mkataba ni siri ya mwajiri na mwajiriwa.Wakati kocha anaajiriwa hatukuonywesha kilichoandikwa ndani ya mkataba licha ya kuonyeshwa kwenye magazeti akisaini.Hatujui vipengere vya mkataba vinasemaje na hata wewe Saleh Jembe huna ubavu wa kutonyesha mkataba wako haha hadharani.Hivyo waachie maumuzi hayo waajiri ndio waliomua kumsimamisha na kumpeleka kwenye kamati ya maadili.Mie niwapongenze Simba kuwa sasa wameanza kuonyesha angalau muelekeo sahihi wa mfumo wa mabadiliko wa kuendesha klabu na kuachana na mihemuko ya mashabiki.
ReplyDeleteAHSANTE AUSSEMS NENDA TU
ReplyDelete