December 10, 2019


Tunaweza kusema mabingwa wa kihistoria katika soka la Tanzania kwa upande wa Ligi Kuu Bara, Yanga, wanapitia wakati mgumu kutokana na madeni wanayodaiwa na wachezaji wao.

Achana na Lamine Moro, David Molinga, Juma Balinya na Sadney Urikhob ambao wanatajwa kuondoka kutokana na kutolipwa stahiki zao, Yanga bado ina mtihani wa Anderw Vicent 'Dante'.

Mtihani unatokana na deni lake la shilingi za Kitanzania, milioni 45 ambazo bado anadai mpaka sasa.

Dante anadai fedha hizo zikiwa zimeunganika zile za mshahara na usajili, mchezaji huyo anaidai Yanga na miezi kadhaa sasa hajafanya kazi ya kuichezea timu yake mpaka alipwe.

Uzito wa madeni ambayo kiuhalisia Yanga imeyumba kiuchumi hivi sasa unaipa wakati mgumu klabu hiyo ambayo ukiachana na Simba, ni kongwe katika soka la Tanzania.

2 COMMENTS:

  1. Uwanja ndio utajengeka na ubingwa wa msimu ni bado wetu kwa kushinda mechi,, zote zilizobaki? 6

    ReplyDelete
  2. Ujinga wa Yanga kukumbatia akina kilomoni hadi kwenye siku ya wanayanga hii ndio faida yake. Wakati Simba wakijitahidi kuepuka matatizo.Yanga wao wanayafurahia bila ya kujua kuwa bila ya uwekezaji mpira wa sasa ni shida.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic