December 24, 2019


KOCHA wa zamani wa Simba, Mbelgiji, Patrick Aussems, amekataa kuzungumza chochote kuhusu Yanga, huku kukiwa na taarifa kuwa klabu hiyo inamtaka awe kocha mkuu kuchukua mikoba ya Mwinyi Zahera.

Kwa sasa Yanga ipo chini ya kocha wa muda Charles Mkwasa lakini mwishoni mwa wiki iliyopita, taarifa za klabu hiyo kuwa katika mazungumzo na Aussems zilishika hatamu katika mitandao ya kijamii.

Hata hivyo, wengi wamezichukulia taarifa hizo kama propaganda za watani kujaribu kuwatoa mchezoni wapinzani wao kuelekea mchezo baina ya timu hiyo, Januari 4.

Simba ilimtimua kocha huyo mwezi uliopita kwa madai ya utovu wa nidhamu pamoja na kuondolewa katika hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo kwa sasa nafasi yake imechukuliwa na Sven Vandenbroeck, raia wa Ubelgiji.

Aussems ameliambia Championi Jumatatu moja kwa moja kutoka Ufaransa kuwa tayari ana ofa sita za kufundisha timu za taifa za Afrika pamoja na klabu lakini anashindwa kuendelea na michakatako hiyo kwa kuwa mwanasheria wake bado hajamalizina na Simba.

“Nipo Ufaransa kwa ajili ya mapumziko kwa sababu bado natafakari kutokana na ofa ambazo mpaka sasa zimekuja lakini siwezi kufanya kitu kwa kuwa mwanasheria wangu bado hajamalizana na Simba.

“Unajua nimeondoka Simba lakini kuna vitu tulikuwa hatujamalizana na nilimuachia mwanasheria wangu ashughulikie ndiyo nasubiria lakini juu ya ofa tayari kuna ofa sita za kufundisha timu za taifa na zote ni Afrika lakini pia zipo klabu zikiwemo za kutoka Asia ila hakuna kinachoendelea kutokana na hilo kukwamisha,” alisema Aussems.

Alipoulizwa juu ya taarifa za kutakiwa na Yanga na tayari ameshakamilisha mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo, alisema kuwa hawezi kusema lolote katika suala hilo kabla ya kukata simu lakini hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakuweza kujibu.

1 COMMENTS:

  1. Sasa kama kakata simu mbona mnaaandika anakwenda yanga ww mwandishi uchwara na hao yanga wenzako mnamtaka huyu uchebe sisi tumemuacha na uwezo wa kumlipa hamna nyinyi kandambili aka vyura wa jangwani poleni mtaishia kumwandika kila kukicha

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic