December 24, 2019


Ofisa Muhamasishaji wa klabu ya Yanga, Antonio Nugaz amefunguka kwa kulitolea ufafanuzi suala la nafasi yake dhidi ya Hassan Bumbuli ambaye ni Ofisa Habari.

Nugaz ameeleza yeye na Bumbuli wamepewa majukumu tofauti yanayowatofautisha kutokana na kazi wanazozifanya.

Ameeleza kuwa majukumu anayoyafanya yeye yanakuwa yanaingiliana na yale ya usemaji sababu mara nyingi amekuwa akiwahabarisha wanayanga juu ya matukio ambayo yanajiri.

Aidha, Nugaz amesema kuna masuala mengine ambayo hawezi kuyazungumzia na badala yake idara iliyo chini ya Bumbuli inahusika.

Ufafanuzi huu ameamua kuutoa kutokana na kuwepo kwa maswali mengi baina ya nafasi yake ndani ya Yanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic