UONGOZI wa Azam FC umeema kuwa kazi kubwa kwenye Kombe la Shirikisho ni kutetea taji hilo ambalo lipo mikononi mwao kwa sasa.
Jana Azam FC ilishinda mchezo wake wa kwanza wa hatua 62 mbele ya African Lyon kwa changamoto ya penalti kwa kushinda penalti 4-1 baada ya dakika 90 kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Uhuru.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa ushindani ni mkubwa kwenye mashindano haya ila Azam wamejipanga kutetea taji lao.
"Kila timu imejipanga kufanya vema hilo lipo wazi ndio maana unaona kwamba hata hawa wapinzani wetu wameonyesha uwezo, tutapambana kuona kwamba tunatetea taji letu," amesema.
hakuna kitu hapo safari hii AZAM mnatolewa mapema tu,mnacheza mpira wakipumbavu kabisa.
ReplyDelete