MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho Azam FC wamepania kutetea taji lao msimu huu kwa kufanya kweli katika mechi yao ya kwanza dhidi ya African Lyon.
Azam FC ilitwaa ubingwa huo kwa kuichapa Lipuli bao 1-0 kwenye mchezo wa fainali bao la ushindi likifungwa na Obrey Chirwa.
Ofisa Habari wa Azam FC, Jaffary Maganga amesema kuwa maandalizi ya kikosi yapo sawa na wanaamini watafanya vema kwenye mchezo wao huo.
"Maandalizi yanaendelea,niwaombe mashabiki tukutane Uwanja wa Uhuru Jumatatu ijayo, tutakapokuwa tukivaana na African Lyon," amesema.
Azam FC inatarajiwa kumenyana na African Lyon, Desemba 23 uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni.
0 COMMENTS:
Post a Comment