NAHODHA wa Simba Queens, Mwanahamis Omary amesema kuwa kikubwa kinachoibeba timu hiyo ni ushirikiano na kufuata maelekezo ya mwalimu.
Jana Simba Queens ilizindua uwanja wa Simba Mo Arena kwa ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Marsh
Queens ikiwa ni mchezo wa kwanza wa ushindani kuchezwa baada ya uwanja huo
uliopo Bunju kuzinduliwa.
"Tunashirikiana kwa ukaribu na kila mmoja, timu inajua nini inataka na wachezaji wanajua nini wanataka, mashabiki watupe sapoti," amesema.
Simba Queens imefikisha jumla ya pointi 13 ikiwa imecheza mechi tano sawa na Alliance FC ambao nao walishinda mabao 2-0 mbele ya Tanzanite.
0 COMMENTS:
Post a Comment