December 29, 2019


Kocha msaidizi wa Azam FC, Iddi Cheche amesema maandalizi na hasira zao kwa sasa wanahamishia kwenye mchezo unaokuja wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Polisi Tanzania.

Mechi hiyo inatarajiwa kuchezwa kesho kwenye uwanja wa Ushirika Moshi. Cheche alitoa kali hiyo juzi baada ya kikosi hicho kufungwa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani Tanga.

Alisema licha ya hali hewa kuwa tofauti kwao lakini sababu kubwa iliyowafanya kushindwa kuibuka na pointi tatu ni baadhi ya wachezaji wa kikosi hicho kucheza chini ya kiwango.

“Nikweli tumepoteza mchezo, pamoja na hali ya hewa ya uwanja lakini baadhi ya wachezaji wetu walicheza chini ya kiwango ambapo walishindwa kufuata maelekezo tuliyowapa kwenda kutekeleza tumekubali matokeo lakini hasira na mipango yetu ni kwa mchezo unaokuja dhidi ya Polisi Tanzania,” alisema Cheche.

Aidha alisema hadi sasa wamepoteza michezo mitatu dhidi ya Simba,Ruvu Shooting na Union hivyo benchi la ufundi lina mtihani mkubwa kwani malengo yao ni kuwania ubingwa hivyo wanajipanga kurekebisha makosa yao ili kujiweka sawa kiushindani.

Naye kocha Juma Mgunda amefurahishwa na ushindi huo kwani kwenye uwanja huo wa nyumbani kwa michezo ya hivi karibuni wamekuwa wakishindwa kuibuka na pointi tatu.

“Nimefurahishwa na ushindi kwa kuwa katika michezo yetu mingi tuliyocheza hapa (Mkwakwani) tumeshindwa kuibuka na ushindi wa pointi tatu kama tulivyofanya leo (juzi),nadhani hali ya kujiamini imerudi kwa wachezaji wangu na sasa watawezekana kupigania ushindi hapa,” alisema Mgunda.

1 COMMENTS:

  1. Hakuna timu hapo mnapoteza pesa mmeenda kununuwa magarasa hayo fukuzeni wote muunde timu mpya kocha mlimfukuza mkamrudisha tena wachezaji walio achwana timu zingine mmewaokota nyinyi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic