December 7, 2019

DOMINIC Calvert-Lewin ameliwasha leo wakati Everton ikiibuka na ushindi wa mabao 3-1 mbele ya Chelsea iliyo chini ya Frank Lampard.

Mabao mawili Dominic alifunga dakika ya 49 na dakika ya 84 huku lile la ufunguzi likipachikwa na Richarlison dakika ya 5.

Bao pekee la kufutia machozi kwa Chelsea lilifungwa na Maleo Kovacic dakika ya 52.

Huu ni mchezo wa kwanza kwa Duncan Ferguson aliyechukua mikoba ya Marco Silva ambaye alipigwa chini mazima kutokana na mwenendo mbovu wa timu.

Sasa Everton inafikisha jumla ya pointi 17 ikiwa nafasi ya 17 huku Chelsea ikiwa nafasi ya nne na ina pointi 29 zote zimecheza mechi 16.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic