December 7, 2019


SPURS imeamua ilipe kisasi leo cha kuchapwa mbele ya Manchester United kwenye mchezo wao uliopita mabao 2-1 wakiwa Old Trafford baada ya kuhamishia hasira zote kwa Burnley FC.

Jose Mourinho kocha mkuu wa Spurs ameshuhudia kikosi hicho kikiichapa mabao 5-0 Burney na kukomba pointi tatu zote.

Mabao kwa upande wa Spurs yalipachikwa na Harry Kane ambaye alipachika mawili dakika ya 4 na 54, huku waliopachika mojamoja wakiwa ni pamoja na Lucas Moura dakika ya 9, Son Heung-Min dakika ya 32 na Moussa Sissoka alipachika msumari wa mwihso dakika ya 74.

Sasa Spurs inakuwa nafasi ya sita na pointi zake 23 huku Byrney ikiwa nafasi ya 14 pointi zake 18 zote zimecheza mechi 16 za Ligi Kuu England.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic