December 7, 2019


MARCUS Rashford mshambuliaji wa Manchester United ana balaa na timu kubwa baada ya leo kuitungua Manchester City bao la kwanza kwa mkwaju wa penalti dakika ya 23.

Bao la pili kwa Manchester United ambayo haikuanza ligi vizuri msimu huu lilipachikwa na Anthony Martial dakika ya 29.

Manchester United ilifunga mabao yote ya mwanzo kipindi cha kwanza na kuwafanya Manchester City ambao ni mabingwa watetezi wa taji la Ligi Kuu England kwenda vyumbani wakiwa na hesabu za kupindua meza.

Rashford aliitungua Spurs mechi ya mwisho Old Trafford kwa penalti bao lake la pili na ulishindi kwa timu yake wakati ikiibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambayo yote aliyajaza kimiani yeye mwenyewe na leo amefungulia kwa penalti.

Kipindi cha pili Nicolas Otamend aliandika bao la kwanza kwa Manchester City dakika ya 85 lililowafuta machozi City.

Ushindi huo unaifanya Manchester United kuwa ndani ya tano bora ikifikisha jumla ya pointi 24 huku City ikiwa nafasi ya tatu na pointi zake 32 na zote zimecheza mechi 16.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic