ZDRAVKO Logarusic raia wa Crotia ambaye aliwahi kuinoa Simba msimu wa 2013/14 na kuibukia timu ya Taifa ya Sudan iliyopigwa chini na Taifa Stars kwenye michuano ya Chan amesema kuwa ameshangazwa na maamuzi ya Simba kumtimua kocha wao Patrick Aussems mapema ilihali ana mafanikio makubwa kwa muda mfupi.
Logarusic ambaye kwa sasa hana timu baada ya kumaliza mkataba na timu ya Sudan amesema kuwa kitendo cha Simba kumtimua Aussems sio cha uungwana kimeendeshwa na mihemuko ya viongozi kwa kutazama upande wa wapinzani wao.
Aussems amefungashiwa virago baada ya kukaa benchi kwenye Ligi Kuu Bara kwenye mechi 10 akishinda 8 sare moja mbele ya Tanzania Prisons na kupoteza moja mbele ya Mwadui FC na Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 25.
“Soka la Afrika lina changamoto kubwa nashangaa kuona Simba inamtimua kocha bila sababu ya msingi kwani alikuwa anaijenga timu na tayari ilikuwa kwenye mfumo ambao ulikuwa umeshajibu sasa sijajua kwa nini wamemtimua.
“Kwa kocha aliyepambana na kuipeleka timu hatua ya robo fainali kwenye Ligi kubwa Afrika kisha anabadilishiwa wachezaji wapya anafukuzwa bado hainipi majibu, labda wawe na sababu binafsi ambazo wanazijua ,” amesema Logarusic.







0 COMMENTS:
Post a Comment