JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa timu ya Yanga amesema kuwa kikubwa ambacho kinawapa ushindi Yanga ni ushirikiano uliopo ndani ya timu pamoja na wachezaji kufuata maelekezo kutoka kwa kocha wao Boniface Mkwasa.
Yanga imeshinda mechi zake zote tatu na kupata sare moja ikiwa chini ya Mkwasa kwa kuanza na Ndanda FC bao 1-0 ikiwa ugenini, JKT Tanzania mabao 3-2 ikiwa uwanja wa Uhuru na ushindi mbele ya Alliance kwa mabao 2-1 uwanja wa CCM Kirumba na imelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na KMC
Akizungumza na Salh Jembe, Abdul amesema kuwa wachezaji wamekuwa na hasira za kupata matokeo kutokana na kazi ambayo wanayo ndani ya ligi kwa sasa.
“Tuna jukumu kubwa la kutafuta matokeo na tunatambua kwamba mashabiki wanahitaji kuona timu inashinda, kocha amekuwa akitujenga kisaikolojia nasi tunafuata kile tunachoambiwa.
“Kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti mambo mazuri yanakuja na wenyewe watapenda kwani kila mchezaji ana morali ya kutafuta ushindi,” alisema.
Yanga ipo nafasi ya 9 ikiwa imecheza mechi 8 imejikusanyia jumla ya pointi 17 imefunga mabao 12 na kufungwa mabao 8.
0 COMMENTS:
Post a Comment