PATRICK Aussems aliyekuwa kocha mkuu wa Simba amesema kuwa hatawasahau mashabiki wa Simba kwa sapoti waliyompa wakati alipokuwa Bongo pamoja na sapoti yao kila kona alipokuwa kwenye ardhi ya Tanzania yenye watu wenye upendo.
Aussems ameondoka leo na kuelekea zake nchini Ubelgiji baada ya kusimamishwa kazi na bodi ya uongozi wa Simba kwa kuwa kile kilichoelezwa kutokuwa na maelewano baina yake na wachezaji.
Kwenye mechi 10 za ligi ambazo ameziongoza Aussems alishinda nane akifungwa mechi moja mbele ya Mwadui FC bao 1-0 na kulazimisha sare moja mbele ya Tanzania Prisons na mchezo wake wa mwisho alishinda mabao 3-0 mbele ya Ruvu Shooting.
"Hakuna kitu kizuri kuwa kwenye ardhi ya Tanzania yenye mashabiki wenye upendo pamoja na ushirikiano ila kwa sasa ninaondoka Bongo na nitakuwa kwenye masuala yangu binafsi zaidi nitawakumbuka kila saa kila wakati," amesema Aussems.
0 COMMENTS:
Post a Comment