MANCHESTER United, imeshauriwa na staa wa zamani wa kikosi hicho Paul Parker kumuuza Kiungo wake Paul Pogba.
Tangu uhamisho wake wa pauni milioni 89 akitokea Juventus Pogba ameshindwa kufurukuta na kuonyesha thamani hiyo na amekuwa akikosolewa kwa kushindwa kujituma.
Kiwango chake kimekuwa cha kupanda na kushuka kila wakati anapokuwa ndani ya uwanja licha ya kwa sasa kusumbuliwa na majeraha.
"Nadhani kama itatokea nafasi ya kurudisha fedha yao wanapaswa kuitumia fedha hiyo kwa busara kwa ajili ya kusajili sehemu zenye udhaifu.
"Anahitaji mabadiliko kwake binafsi na afya ya klabu pengine ni vyema akaondoka," amesema Parker ambaye alitwaa ubingwa wa Premier mara mbili akiwa na Manchester United.








0 COMMENTS:
Post a Comment