December 7, 2019


MASHABIKI wa Simba leo Desemba 7 wamealikwa na uongozi wa Simba kutembelea maeneo ya Bunju ambapo kuna viwanja viwili vya mazoezi vilivyo kwenye hatua za mwisho kukamilika kabla ya kuanza kutumika rasmi kwa mazoezi.

Simba imejenga viwanja viwili vya mazoezi ambapo kiwanja kimoja ni cha nyasi bandia huku kingine kikiwa ni cha nyasi asilia na pia kuna vyoo na sehemu za kubadilishia nguo ambazo zimekamilika kwa asilimia kubwa.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa lengo kubwa ni kuona timu inafikia malengo makubwa ambayo yamewekwa hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi leo kuona namna kazi inavyokwenda.

Edward Shirima, ambaye ni mkandarasi na msimamizi wa mradi huo amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa.

"Kwa sasa tupo kwenye hatua za mwisho kuukamilisha mradi huu ambao umekuwa na mafanikio makubwa, imani yetu kila mmoja atapenda kwa namna ambavyo tumefanya kazi kwa umakini bila longolongo yoyote," amesema. 

3 COMMENTS:

  1. Replies
    1. ha ha ha, big club ndio mikia fc kweli jamani?

      Delete
  2. Wapuuzi FC wanashindwa hata kulipa mishahara ya wachezaji.Mmezoea kuwadhulumu kina Dante sasa upele umepata mkunaji.Vyura mtakoma.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic