Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba jana wameendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na Kombe la Shirikisho la Soka nchini maarufu FA Cup dhidi ya Arusha United pamoja na michezo ya Ligi Kuu.
Kutokana na mabadiliko ya ratiba ya Ligi Kuu Bara yaliyofanywa na Bodi ya Ligi hivi karibuni, Simba itacheza mechi tatu Uwanja wa Uhuru kabla ya Januari 4, mwakani kuvaana na Yanga katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Baada ya kuikaribisha Arusha United kwenye mechi ya Kombe la FA, Desemba 25 itavaana na Lipuli FC huku siku tatu baadaye ikiwa na kibarua kigumu dhidi ya KMC FC kabla ya kufunga mwaka kwa kuikaribisha Ndanda FC hapo Desemba 31, mwaka huu.
Kocha Msaidizi wa Simba, Selemani Matola alisema wachezaji wa kikosi hicho wapo vizuri wakati huu wakiendelea na mazoezi na kufafanua kuwa kila kitu kinakwenda sawa.
"Tunaendelea vizuri na mazoezi kwa ajili ya Kombe la Shirikisho pamoja na mashindano ya Ligi Kuu," alisema Matola ambaye ataanza kukiongoza kikosi hicho kwa mara ya kwanza msimu huu akiwa na Kocha Mkuu Mbelgiji Sven Vandenbroeck baada ya
Patrick Aussems kutimuliwa.
Naye msemaji wa klabu hiyo, Haji Manara akizungumzia usajili wa dirisha dogo, alisema kwa upande wao hawana pupa na kudai watasajili kwa matakwa ya kocha wao ambaye anaendelea kukisoma kikosi hicho baada ya kukikabidhiwa hivi karibuni.
Alisema endapo kocha atahitaji kuongeza au kupunguza mchezaji yeyote, watasajili na kudai wapo imara idara zote kwa sasa.
"Sisi hatuna pupa ya usajili tutasajili kwa matakwa ya kocha wetu hatusajili kwa ajili ya kufurahisha watu," alisema Manara.
Aliendelea kusema wanaendelea kujipanga kwa ajili ya kukutana na mahasimu wao Yanga, Januari 4 Mwakani.
"Yanga wasajili kila siku, lakini tukutane Januari 4 Taifa," alisema.
kwakweli yanga wajiandae kisakolojia
ReplyDeleteWewe na huyo mwehu wenu nyote hamna akili kabisa mbona yanga wanafanya yao kivyao kwanini na nyie msipambane na hali zenu tu
ReplyDeleteMKUBALI TU KWENYE USAJILI YAGA WAKO VIZURI SANA KU;ENGA WACHEZAJI KULIKO SIMBA
ReplyDeleteSubirini majibu uzuri wa timu ni matokeo na sio kusajili tu,wamecheza ngapi?wameshapoteza ngapi?wamedroo ngapi?na ushindi ngapi?wana magoli mangapi yakufungwa nakufunga?hapo ndipo mahali pekee patakapo dhihirisha nani yuko vizuri,yanga wanatumia personal sucrifying yani mchezaji anasajiliwa na yanga,but analipwa kila kitu na rogers kwa lengo lakuitumikia yanga,janja yenu inajulikana sana,chamsingi igeni mfumo wa simba mbona mnaweza sana,mnajitisha wenyewe,watu wanaelewa kila kitu wachezaji wengi hapo wanalipwa na watu binafsi au tuseme wanachama wenye mapenzi na timu yao.na ndiomana inapokuja club inapishana kidogo na mwanachama ambae anamlipia mcheza mishahara lazima kinuke,chamsingi fuaten mfumo wa simba wanachama wapewe hisa zao wapate asilimia zitakazo wawezesha kushiriki kwenye zoezi lakununua au kusajili wachezaji.
ReplyDeleteRogers ni kama sample tu,wapo wengi sana hapo yanga wanaojitoa kwa ajili ya yanga ndiomana mnashauriwa kuiga mfumo wa simba,na endapo mtakubali kufanya hivyo basi yanga mtafanikiwa kwa haraka sana kuliko simba,mtu hawezi kukubali kuwekeza pesa bila yakuandikishana hisa na mkataba uwepo mezani ili kila mtu ajiridhishe wengi ya wanachama wa yanga wanaogopa nakuhofia kupoteza pesa zao kwasababu ya mfumo mbovu wakuendesha timu.
ReplyDeleteLeo mnakula matapishi yenu nyinyi kandambili aka vyura wa jangwani
ReplyDeleteKati ya usajili waliosema wa kutisha wa Yanga ni wa kabla ya ligi kuanza,sijui nini kimewatokea na sasa wanapayuka tu na majina ya wachezaji.
ReplyDelete