PATRICK Aussems aliyekuwa kocha mkuu wa Simba amesema kuwa ilikuwa ngumu kwake kufanya kazi ndani ya Simba kutokana na kuwekewa vikwazo vingi na watu wa bodi ya ligi ambao walikuwa hawampi ushirikiano katika yale anayoyataka.
Aussems amefukuzwa ndani ya Simba baada ya kisimamia kwenye jumla ya mechi 10 za ligi akishinda nane na kupata sare moja mbele ya Tanzania Prisons huku akifungwa na Mwadui FC bao 1-0.
Aussems amesema kuwa kuna mambo ambayo yalikuwa yanatokea ndani ya Simba alikuwa hayaelewi ila mwisho wa siku alipambana kusimamia haki.
"Hakukuwa na mpangilio mzuri katika mawasiliano hasa na bodi ila yote ni kheri kwani nimefurahi kuwa ndani ya Simba pamoja na ardhi ya Tanzania, umakini na usahihi katika maamuzi unatakiwa ndani ya Simba kufikia mafanikio.
"Unajua haina maana kwamba wachezaji wote ambao nilikuwa nao niliwahitaji hapana pia kuna mengi ambayo yanapaswa yafanyiwe kazi ndani ya Simba ili kufikia malengo ambayo wanayafikiria," amesema.
Kwa sasa mchakato wa kumtafuta kocha unaendelea ndani ya Simba huku habari zikieleza kwamba anahitajika kocha kutoka bara la Afrika na sio mgeni kuja kuinoa timu ya Simba iliyotinga hatua ya robo Fainai Ligi ya Mbingwa msimu uliopita.







Mnafiki mkubwaa sepa zako tuachie timu yetu
ReplyDeletendio maana nilisema patrick hakupewa nafasi ya kujitetea,sasa hayo ni baadhi tu ya malalamiko yake,all in all simba mmechemka na am sure mtajutia maamuzi hayo,
ReplyDeleteHakuna cha kujutia.haiwezekani bodi ya wajumbe zaidi ya kumi na nwekezaji MO wasitishe mkataba bila sababu.Tunda linaweza kuwa zuri kwa nje lkn ukilikata unakuta limeharibika na huwezi kulila zaidi ya kulitupa.Mashabiki tusijifanye tunajua Zaidi ya viongozi au basi hakuna maana ya kuchagua viongozi.Kuhusu wachezaji kuwa wote hawakuwa chaguo lake basi kwa nini asingejiuzulu na kutoa sababu ambazo wadau wa soka tungemuelewa. Tahadhari na ushauri kwa wajumbe wa bodi ni kuwa makini sana na mchakato wa kupata kocha aliye bora zaidi ya Aussems au la sivyo kesho na keshokutwa wasikimbie kubeba msalaba waliojivisha sasa.vinginevyo hakitaeleweka
DeleteHaya wacha tuone huyo atakae kuja sijui kama tutachukuwa huwo ubingwa wa ligi kuu
ReplyDeleteKinachoonekana kwa Patrick Ausems kwa sasa ni kuweweseka.Maneno mengi hayatamsadia wala hayata wasaidia Simba.Mpira ni mchezo wa hadharani na vitendo ndivyo vinavyoongea zaidi kuliko blah blah. Kazi ya Ausems pale Simba haikuwa kusumbuana na viongozi bali ni kuonesha utaalamu wake uwanjani.Tatizo kubwa nililoliona kati ya Ausems na Simba ni kwamba kila mmoja kati yao walikuwa na mtazamo na malengo tofauti yaani Ausems aliichukulia Simba poa tu yaani ni katimu kadogo yaani hata yeye mwenyewe binafsi alihisi ni mkubwa kuliko Simba. Kwa upande wa uongozi wa simba wengi wao walikuwa na mawazo tofauti na Ausems kwani wanaamini Simba ni timu kubwa kariba za kina Mazembe,Alhaly,Esperence ya Tunisia na vigogo vengine vya barani Africa na kwa kuchukulia umri wa Simba na ukubwa wa mtandao wa wanachama wao hakuna ubishi kweli Simba sio timu ndogo ila kimafanikio hasa kwa ngazi ya kimataifa kweli Simba ni timu changa na hapo ndipo kunakowakwaza viongozi wa Simba. Wanakesha na kuhaha wakiwaza vipi wataibadilisha hali hiyo ya Simba yakuwa timu ya kawaida barani Africa nakuwa timu mshindani wa kweli? na Ausems sio kocha wa gharama ndogo hata kidogo ni miongoni mwa makocha ghali Tanzania pengine Africa na kama kocha ghali basi watanzania tusiwe wapumbavu kwani Simba ni kampuni na kampuni haiwezi kuwa na malengo ya kujiendesha kwa hasara. Fikiria Aussems amewakosesha Simba mamilioni mangapi baada ya Simba kutolewa hatua ya awali kwenye klabu bingwa Africa? Bado Simba inahitaji sana mchango wa wanachama wao wanaokwenda kulipa viingilio uwanjani na kama kutaongeongezeka fungu la pesa kutoka maendeleo ya soka Africa CAF baada ya timu kufanya vizuri basi ni faida zaidi kwa timu. Ila sijawahi kumsikia Aussems akiomba radhi wanasimba hadharani baada ya timu kufanya vibaya klabu bingwa Africa. Na Ausems alitakiwa kufahamu yakwamba ushiriki wa Simba klabu bingwa Africa si tu mwakilishi wa nchi bali mashindano yale ni moja ya biashara mama yakampuni ya Simba yaani ndio malengo ya Simba kwa sasa na hata gharama za uendeshaji wa timu zinategemea kwa kiasi fulani ushiriki mzuri wa mashindano hayo makubwa barani Africa. Sasa kwa Ausems kuyachukulia poa tu mashindano hayo kwa kweli hata mimi ilikuwa inanikera. Yaani Simba kapigwa tano mtungi halafu kocha hata presha hana na kama vile haitoshi anakuja kupigwa tena tano kavu halafu tena hata kukereka hakereki? Nadhani baada ya kuwaalaumu viongozi wa Simba Ausems alitakiwa kuwashukuru sana viongozi wa Simba kwa kumpa nafasi lakini kubwa kwa kumvumilia la sivyo alipaswa kufukuzwa zamani sana pale simba.
ReplyDeleteAussie twende zanzibar tukaloge sitaki nataka hapa gymkana watu wakamwaga na hivi mshahara ni mamilioni na nyie hamtaki kumwachie mo mijengo yote ya simba acha alipe hawa wa mafungu kina matola si ndio soka letu huyo mwambie nendeni mligoti anaenda hana shida mzugu unaanzaje kumpeleka
ReplyDeleteZahera waliroga na Yanga lakini haikumsadia kufukzwa bila ya kulipwa stahiki zake Yanga hovyo kabisa.
ReplyDelete