December 28, 2019


Kocha wa muda wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema kuwa anaamini watawafunga Simba katika mchezo wa Januari nne, mwakani kwa kuwa safu yake ya ushambuliaji imeshaanza kupika mabao.

Mkwasa amesema tatizo kubwa ambalo lilikuwa linaisumbua timu yake ni kushindwa kutengeneza nafasi za mabao, jambo ambalo amelifanyia kazi na limeanza kuzaa matunda.

Yanga walipata ushindi wa mabao 4-0 katika mchezo wa FA waliocheza kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar, Jumamosi iliyopita dhidi ya Iringa United kisha wakasuluhu dhidi ya Mbeya City huku Uwanja wa Sokine ukiwa siyo rafiki kutokana na mvua kubwa iliyonyesha uwanjani hapo.

Mkwasa alisema Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo timu nyingine, kwa kuwa shida kubwa ambayo ilikuwa inaisumbua klabu hiyo ni kushindwa kufunga mabao jambo ambalo wamelifanyia kazi na watapata mabao katika kila mchezo, ukiwemo huo wa Simba.

“Simba ni timu ya kawaida kama zilivyo timu nyingine, tulikuwa na tatizo la kushindwa kupata mabao kwenye safu yetu ya ushambuliaji, tatizo ambalo kwa sasa limepatiwa ufumbuzi, kwa hiyo lengo letu ni kushinda katika kila mchezo hadi huo wa Januari nne,” alisema Mkwasa.

8 COMMENTS:

  1. Hayo mabao wamefunga timu ipi?°!Iringa United???Timu yetu bado dhaifu sana ushambuliaji.Tuseme ukweli. Bila mabeki kucheza vizuri tungefu ngwa na Prisons leo.Tujenge timu tuache maneno.

    ReplyDelete
  2. Bora Mkwasa aedelee kuwa kocha kwakuipa Yanga ushindi na kufanya timu ipige jump mpaka nafasi ya tatu na kukaribia kuukamata mkia

    ReplyDelete
  3. Sasa wewe mkwasa kweli kichekesho,unatuambia safu yako imeshaanza kupika mabao wakati wezako sasa hivi hayo mabao wanayapakua kabisa maana wakati wewe una goli sijui kumi mwezio ana mara mbili yako.

    ReplyDelete
  4. hii sasa kichekesho wameanza kufunga yan mmm

    ReplyDelete
  5. waminishe watu ujinga kwamba utaifunga simba kwa timu ipi? yanga ya manji iliishindwa simba iwe hii ya njaaa kali?

    ReplyDelete
    Replies
    1. huna kumbukumbu wewe, yanga ya manji ilimpiga simba round zote 2 kwenye ligi au nikukumbusehe magoli yalipatkanaje na ni akina nani walifunga?. funika bakuli lako kama huna takwimu.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic