December 28, 2019


Klabu ya Yanga imeeleza masikitiko yake kufuatia kuhamishwa kwa mchezo wao wa ligi dhidi ya Tanzania Prisons kutoka Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya hadi Uwanja wa Samora mjini Iringa.

Mchezo ulihamishwa kutokana na kuharibiwa kwa Uwanja wa Sokoine kufuatia tamasha la muziki lililofanyika katika uwanja huo usiku wa Disemba 25, ambapo uongozi wa Yanga umelalamikia gharama ambazo umetumia kuelekea mchezo huo.

Akizungumza baada ya kuhamishwa kwa mchezo huo, Afisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema, “tutawaandikia barua Bodi ya Ligi ili tujue kama gharama hizi atazibeba nani, tutahoji baada ya kupitia kanuni zinasemaje lakini hakukuwa na ulazima wa kulazimisha mchezo huu kuchezwa”.

“Hivi vitu sio vya kukaa kimya, sisi tumefika Iringa saa saba usiku na Tanzania Prisons wamefika saa 3 Usiku na tumetumia gharama kubwa pale zaidi ya milioni 18 ambayo ni milioni 6 ka siku na tumekaa zaidi ya siku tatu”, ameongeza Bumbuli.

3 COMMENTS:

  1. sasa tofauti iko wapi iringa ni njiani kwenda dar garama zipi zimeongezeka prison ndo waombe garama za kutoka mbeya iringa mbeya.Garama za iringa walikuwa watumie mbeya

    ReplyDelete
  2. umasikini nishida kweli sasa unalalamika wakati ndo ushaanza kurudi nyumbani jaman tunakwama wapi yanga hebu tuache makelele tujipange kiushindani uwanjani na siomdomoni!!

    ReplyDelete
  3. Acha kuropoka we unadhani yanga ulijuwa iko dar ???? Au unaongea ujui kitu

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic