December 28, 2019


Baada ya kufanikiwa kuibuka na ushindi wa bao 1-0dhidi ya Tanzania Prisons jana lililowekwa kimiani na kiungo fundi Patrick Sibomana katika dakika ya tano tu ya mchezo, uongozi wa Yanga umeshangazwa na mapokezi waliyofanyiwa mjini Iringa.


Yanga iliibuka na ushindi huo ambao uliifanya ipande kileleni mpaka nafasi ya tatu kwa kufikisha jumla ya alama 21 ikiwa imecheza michezo 10.


Kutokana na mapokezi hayo juzi mjini humo, Ofisa Uhamasishaji wa klabu hiyo, Antonio Nugaz, ameeleza kushangazwa na mapokezi hayo akiyafananisha na namna Rais wa Tanzania, John Pombe Magufuli ambavyo amekuwa akipokelewa pindi anapofanya ziara zake mikoani.

Nugaz amesema ameshangazwa na namna jina la Yanga lilivyo kubwa baada ya kwenda na kikosi cha timu mjini humo na mamia ya amshabiki kujitokeza kwa wingi wakiipokea timu kwa mechi hiyo ya Ligi Kuu Bara.

"Kiukweli nimeshangazwa na ukubwa wa timu ya Yanga, haya mapokezi tuliyofanyiwa huku ni kama msafara wa Rais Magufuli ambavyo amekuwa akipokelewa.

"Kwa sasa tunajipanga kwa ajili ya mechi zijazo ikiwemo dhidi ya Biashara ambayo ndiyo inafuata," amesema Nugaz.

3 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic