December 12, 2019


Timu ya Simba na Yanga watacheza mechi zao la Ligi Kuu Tanzania Bara katika siku kuu Krismasi kwa mujibu wa ratiba mpya ya ligi hiyo kabla ya mchezo wao wa watani wa jadi utakaopigwa Januari 4, 2020.

Awali ratiba ya Ligi Kuu ilikuwa inaonyesha Simba, Yanga na Azam hazitokuwa na mchezo wowote mpaka mwakani, lakini kwa mujibu wa ratiba mpya iliyotolewa Bodi ya Ligi inaonyesha watacheza mechi mbili kila moja kabla ya kufunga mwaka.

Kwa mujibu wa ratiba inayonyesha Desemba 24, Yanga watakuwa jijini Mbeya kucheza dhidi ya Mbeya City wakati mabingwa wa Ligi Kuu Bara wenyewe watashuka uwanja siku ya Krismasi Desemba 25 kuivaa Lipuli kwenye Uwanja wa Uhuru.

Yanga watashuka tena kwenye Uwanja wa Sokoine, Desemba 27 kuivaa Tanzania Prisons wakati Desemba 28, KMC watakuwa wenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa Uhuru.

Baada ya hapo Simba na Yanga zitapata wiki moja ya kujianda kwa kabla ya mchezo wao wa watani wa jadi utakaopigwa Januari 4, kwenye Uwanja wa Taifa.

Mabingwa wa Kombe la FA, Azam watakuwa wageni wa Polisi Tanzania Desemba 24, na siku tatu baadaye watasafiri hadi Tanga kuivaa Coastal Union kwenye Uwanja wa Mkwakwani Desemba 27.

2 COMMENTS:

  1. Kuvunja Mikataba Wakati Ligi Inaendelea na Unakabiliwa na Mechi za Viporo
    Unajua nashindwa kuelewa nia na adhma ya Uongozi wa Yanga unapochukua baadhi ya Maamuzi ambayo mengine ni ya ajabu...huku ligi ikiendelea na dirisha dogo la usajili halijafunguliwa na Timu ina mechi za ligi na viporo, Mapinduzi Cup, na FA Cup

    Cha ajabu wachezaji mastraika wote wameondoka na hakuna mshambuliaji aliyebaki zaidi ya Molinga na Sibomana, sasa sifahamu nia ni ipi...Je Yanga itacheza mechi zake bila ya wachezaji hawa wafuatao ambao ni washambuliaji
    1. Sadney Urikhob
    2. Juma Balinya
    3. Maybin Kalengo
    Hata kama wachezaji mbadala watasajiliwa...hawataruhusiwa kucheza mpaka wapitishwe na TFF kuanzia mwezi 1 tarehe 20..sifahamu wahusika wameliona hili au vipi?
    Nina wasiwasi na Viongozi wa Yanga.....katika nia zao moyoni ni zipi? Dhana ya kwamba wamepenyezwa na maadui (Simba) inaweza ikawa kweli!....mwenye nia ya dhati na kutaka maendeleo ya timu hawezi kuchukua maamuzi mapema wakati ligi inaendelea na timu inakabiliwa na mechi muhimu ikiwemo na watani wa jadi!
    Tafadhalini Viongozi wa Yanga msilete migogoro kwa maamuzi ya pupa pasipo kuchambua hali ya mambo ilivyo...badala ya kujenga mtaanza kubomoa. Nadhani Simba Sports Club inaendeshwa kisayansi na kisasa zaidi na CEO mpya kuliko Yanga....wao wanaendesha kwa kisiasa na kiswahili!

    Ahsanteni

    ReplyDelete
    Replies
    1. Yanga hawaja jpanga, kuacha wachezaji ni kwa sababu ya ukata, unasajili vipi wakati huna hela???? kw maana hio utajikuta unasajili wachezaji cheap cheap na wenye uwezo wa kawaida, inabidi wajipange upya.... Hali si shwari kabisaaaa

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic