AMRI Said, Kocha Mkuu wa Mbeya City amesema kuwa kwa sasa mpango mkubwa ni kusajili mashine sita za kazi ambazo zitarejesha heshima kwenye kikosi hicho cha Mbeya City.
Said amechukua mikoba ya Juma Mwambusi ambaye alijiuzulu kutokana na kuwa na mwenendo mbovu wa timu hiyo akiwa ameshinda mechi moja tu kati ya mechi 12 alizosimamia.
"Nimeona kikosi kina tatizo kidogo hasa kwenye safu ya ushambuliaji na ulinzi jambo ambalo linafanya timu isiwe na matokeo chanya ila nina amini nikipata wachezaji sita tutakuwa katika reli ya ushindi," amesema.
Miongoni mwa wachezaji wanaowindwa na Mbeya City ni pamoja na Abdulmajid Mangalo na Ally Kombo wote walifundishwa na Said alipokuwa Biashara United.
0 COMMENTS:
Post a Comment