BONIFACE Mkwasa, Kaimu Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa leo atawatumia nyota wake wote wa kikosi cha kwanza kuimaliza Iringa United kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho utakaochezwa uwanja wa Uhuru.
Yanga leo itatupa kete yake ya kwanza kwenye michuano ya Kombe la Shirikisho na itamenyana na Iringa United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza kusaka tiketi ya kusonga mbele hatua inayofuata.
Mkwasa amesema:" Siwatambui vema wapinzani wangu Iringa United ila nitashusha kikosi kazi chote uwanjani ili kutafuta ushindi kwani nina amini utakuwa mchezo mgumu na kila timu inahitaji ushindi.
"Maandalizi yetu yapo sawa na kila mchezaji anatambua jukumu lake nina amini tutafanya vizuri ili kusonga mbele kwenye hatua inayofuata," amesema.
Bingwa wa Kombe la Shirikisho atapata nafasi ya kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya kimataifa ya Kombe la Shirikisho Afrika na kwa sasa kombe lipo mikononi mwa Azam FC.
0 COMMENTS:
Post a Comment