December 13, 2019


Msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara, amefunguka kuwa yeyote anayesema kuhusu kuonewa na kufukuzwa kwa aliyekuwa kocha wao Patrick Aussems, basi amfuate hukohuko alipoenda.

Haji Manara amejibu hivyo kupitia EATV & EA Radio Digital, baada ya kuwepo na maoni mengi ya mashabiki wa klabu hiyo ya Simba, kusema kocha aliyefukuzwa ghafla hakustahili kufanyiwa hivyo.

"Kwa maana hiyo mnataka mseme Mohammed Dewji anayelipa pesa awe haipendi Simba na anamuonea, yaani pesa ziwe zake halafu awe anamuonea huyo mtu, yeye ndiyo mwenyekiti wa bodi utasemaje amtetee mtu ambaye hayupo, tuungeni mkono, twendeni kwenye mpira tuna mechi na Yanga  pia tuna mechi kwenye Kombe la FA" ameeleza Haji Manara.

Aidha Haji Manara ameendelea kusema "Tutakwenda kuchukua ubingwa wetu, mimi nitaondoka, Aussems kaondoka, wataondoka wengine na wengine ila Simba itabakia palepale na itaendelea kuwepo, kama uliipenda Simba kwa ajili ya Aussems mfuate Aussems".

Klabu ya Simba siku ya Disemba 11, 2019, ilimtambulisha kocha wao mpya aitwaye Sven Vanderbroeck, raia wa Ubelgiji, na kocha msaidizi aliyetambulishwa ni mzawa Selemani Matola.

6 COMMENTS:

  1. Kuna maneno ya kweli lakini hayapaswi kutamkwa kwa nyodo na kejeli. Haji amekuwa akipotoka mara kwa mara nadhani anapaswa kurekebisha mtiririko wa maneno yake ili awiane n ustaarabu wa maoni. Hao ni mashabiki na hawakosi kuwa na nyongo je baada ya Patrick kuondoka timu ikipata matokeo hasi Haji atawaambia nini hao anaowakejeli leo? Je hawatamzomea na kumtupia machupa chakavu? Ajue mashabiki wana nyongo na wanapenda mafanikio wanayoyaona si mapungufu wasiyoyaona.

    ReplyDelete
  2. kila kilicho bora hakikosi kasoro,uchebe ni kocha mzuri...lakini huwa hana plan B kusaka matokeo...ilo ndio tatizo kubwa.

    ReplyDelete
  3. Usitukane Mkunga wakati uzazi ungalipo,je ikitokea huyu kocha mgeni mambi yasipoenda vizuri itakuwaje,hata aussems alimuita Proffessor Leo hafai kitu

    ReplyDelete
  4. Siwezi kushangaa kauli yake kwani hana tofauti na mtoto wa kike,Uchebe yupo juu

    ReplyDelete
  5. jaman hata mm kusema kweli huyu kocha kwa rekod zake tu naona hata hazitishi na hazitoshi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic