LEO timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimajaro Stars iliyo chini ya Juma Mgunda na Zuber Katwila itakuwa kazini kumenyana na Kenya mchezo wa kwanza kwenye michuano ya Afrika Mashariki na Kati (Cecafa Chalenji)
Michuano hiyo inafanyika nchini Uganda na Kilimanjaro Stars itarusha kete yake ya kwanza leo Desemba 7 dhidi ya Uganda kabla ya Desemba 10 kukutana na ndugu zao Zanzibar.
Juma Abdul, beki wa kulia mwenye uwezo wa kupandisha mashambulizi alisema kuwa morali ya wachezaji ni kubwa na kila mmoja anahitaji kupata ushindi.
“Tumejipanga vema na tumefanya maandalizi kiujumla, kila mchezaji anahitaji kuona timu inashinda, mchezo wa mpira ni ushindani tunawaheshimu wapinzani wetu tunajua kwamba nao wamejipanga kama sisi hivyo hatutawadharau,” amesema.
David Kisu mlinda mlango amesema kuwa wana imani ya kupata matokeo kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya kwa muda mrefu.
“Tumekuwa pamoja kwa muda mrefu jambo hili limetuongezea uwezo na morali, kila mchezaji anatambua kwamba taifa linatutegemea hivyo hatutawaangusha,” amesema.
Bakari Mwamnyeto amesema kuwa ni suala la muda tu wao kupambana hivyo watanzania waipe sapoti timu yao.







U can't be serious is it Uganda?
ReplyDelete