December 8, 2019


Baada ya kuibuka kwa taarifa za wachezaji wake wanne kueleza kuidai klabu ya Yanga, uongozi wa klabu hiyo umesema utalitolea ufafanuzi suala hilo.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa klabu, Hassan Bumbuli, amesema kuwa wao kama taasisi wana utaratibu maalum wa kutoa taarifa zao.

Ameeleza kwa kuwataka wanayanga watulie kunako kipindi hiki kwani kila mtu atakuwa anasema na badala yake watakuja na ufafanuzi ndani ya siku kadhaa sijazo.

Wachezaji ambao wanaelezwa kudai na wameandika barua ya kuvunja mkataba na Yanga ni Lamine Moro, David Molinga, Sadney Urikhob na Juma Balinya.

7 COMMENTS:

  1. Iikowapi tamko. Yote haya sababu Yake kujivurumishia bila ya mpango

    ReplyDelete
  2. Yanga anzisheni kampuni ya hisa na kila shabiki na mwanachama ahamasishwe kununua hisa na kila hisa moja iuzwe kwa shilingi elfu kumi 10,000 mpango huu wa uuzaji wa hisa upewe kipindi cha miezi 6 na utaratibu wa ununuaji wa hisa uwashirikishe kampuni ya selecom pay kupitia tigo pesa mpesa airtel money halopesa na zantel na matangazo ya uuzaji wa hisa yafanyike kupitia radio na television na mitandao ya kijamii nchi nzima. Endapo mashabiki milioni moja kati ya watanzania milioni 55 watanunua hisa ndani ya kipindi cha miezi 6 kampuni ya hisa ya yanga itapata shilingi bilioni 100 kupitia fedha hizi yanga itakuwa imepata mtaji wa kuanzisha kampuni au mradi wowote wa kujiingizia mapato bila kutegemea ufadhili au msaada wa mtu mmoja. Na kampuni hii itakuwa inagawa faida kwa wanahisa kila baada ya mwaka mmoja kutegemeana na idadi ya hisa za kila mwanachama. Mfano wanaweza kuanzisha kampuni ya kubeti (sport betting) ni biashara yenye faida kubwa na inaziingizia kampuni hizi pesa nyingi kila siku.Kampuni hii ndio itakuwa inaihudumia timu ya mpira wa miguu ya Yanga ikiwa ni pamoja na kusajili wachezaji na kuwalipa mishahara na stahiki zao. Ni wazo nawasilisha.

    ReplyDelete
  3. Tatizo hata ukichangia ulaji mwingi hamna kinachoendelea wapeleke timu kwa mtindo Wa kisasa Wa kibiashara tu.huku kwingine kudanganyana tu

    ReplyDelete
  4. Zahera aliposema kuna tatizo la uongozi na matumizi ya mabaya isivyokusudiwa alisemwa anaingilia timu. Tochi iliyomulika Ya kina Malinzi na ya Aveva na Kaburu inapaswa ipite Yanga ili KUBWA KULIKO IJULIKANE FEDHA ZILITUMIKAJE ILI KUNUSURU TIMU YA WANANCHI

    ReplyDelete
  5. MASWALI KUIHUSU YANGA

    1. Uchaguzi wa Viongozi wa Yanga....Je, ni kweli kuwa kuna Mamluki kupenyezwa?....Na kweli kwamba hili linahitaji uchunguzi, ushahidi na tafiti kulibaini?
    2. Serikali kutia mkono wake kuipeleleza na kuidhoofisha Yanga, ikiungana na nguvu ya kiuchumi iliyopo Simba...Je, hoja hii ina ukweli ama zimebaki kuwa ni tetesi tu?
    3. Jiulize ni kwanini Klabu ina Wadhamini zaidi ya 4 (SportPesa, Azam TV, Maji ya Afya, GSM Foam, GSM Tanzania & Taifa Gas) lakini kwa misimu miwili mfululizo wachezaji wa Yanga wanalalamikia mishahara? Je, kwanini iwe ni Yanga pekee matatizo haya yanaanikwa hadharani? Je, ni kweli kuwa Vyombo Vya Habari vinatumika kutokana na maslahi ya kiuchumi inayopata kupitia watu wenye nguvu ya kiuchumi na ushawishi mkubwa katika jamii kuichafua Yanga?
    4. Kuwepo kwa Makundi ya wanachama wanaotoka katika makundi yenye maslahi binafsi, na wapiga dili waliokuwepo kutokea msimu uliopita...na kupenyezwa kwa mamluki na wanachama kupitia kwenye kamati lukuki zilizoundwa na Mwenyekiti (ambaye amepoteza support kutoka kwa wapenzi wa Yanga walio sehemu kubwa na wengi wanahoji uhalali wake na moyo wa ushabiki kuwa ni wa Simba)
    5. Wanachama wenye uwezo wa Kifedha waliokuwapo kipindi cha Utawala wa Manji kutotoa Ushirikiano kwa Maslahi ya Yanga kwakuwa Wanaona wanaoongoza Yanga sasa hivi kwamba labda sio waaminifu au hawawakubali kwa namna ambavyo mambo yanavyoendeshwa?
    5. Kuchelewa kwa mfumo wa mabadiliko na uwekezaji, ujenzi wa miundo mbinu kama viwanja vya mazoezi....hapa unajiuliza kwanini ni Yanga tu katika timu hizi 2 kubwa kuna kusuasua? Je, ni jitihada za Serikali ya Awamu ya 5 kuidhoofisha kwa manufaa ya Klabu nyingine ya mtaa wa 2, kwakuwa asilimia kubwa ya Viongozi serikalini wana mapenzi nayo? Au ni udhaifu wa Viongozi wa Yanga? Je, ni kweli kuwa wawekezaji wenye nia ya dhati na walio fedha wanaogopa kuwekeza Yanga kwa kuogopa kuandamwa na vurugu ya Serikali ya Awamu ya 5? Kama ni hivyo, Serikali haioni kuwa hawawatendei haki raia wenye utashi binafsi na mapenzi yao binafsi kwa ustawi wa haki na jamii yenye misingi ya upendo na undugu?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Serikali unaisingizia tu pambaneni na matokeo ya kuachia fursa ya kuibinafaisha klabu yenu na kuishia kujidai mnaweza kuiendesha kwa makusanyo ya michango (bakuri) ya wanaachama wenu na mashabiki .

      Mkataba wa sportspesa nahisi mliishavuta hela yote Sasa mnamtumikia baniani

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic