January 30, 2020

UONGOZI wa timu ya Arusha umesema kuwa makosa waliyofanya kwenye mchezo dhidi ya Gwambina FC hayajatajirudia tena kwenye mechi yao inayofuata dhidi ya Pamba FC wanajipanga kuwapiga mabao kwa hasira.

AFC ilichapwa mabao 3-1 na Gwambina mchezo wao wa Ligi Daraja la Kwanza mchezo wao unaofuata ni dhidi ya Pamba FC utakaochezwa Februari, Mosi, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid.

Ofisa Habari wa AFC, Bahati Msilu amesema kuwa walijifunza kupitia makosa waliyoyafanya na sasa wanajipanga kupata ushindi mbele ya Pamba FC kwa hasira za kupoteza.

“Tulipoteza mchezo wetu uliopita, tuna hasira na wapinzani wetu lazima tupambane kupata matokeo mazuri ndani ya Uwanja, mashabiki watupe sapoti katika hili,” amesema Msilu.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic