January 30, 2020


MICAH Richard, mchezaji wa zamani wa Manchester City amesema kuwa mfumo alioutumia Kocha Mkuu wa City, Pep Guardiola ulimponza mbele ya Manchester United na kukubali kufungwa bao 1-0 mbele ya Manchester United.
Usiku wa Jumatano,Januari 29, City ilikubali kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa wapinzani wao wakubwa Manchester United na bao pekee la ushindi lilifungwa na Nemanja Matic aliyefunga bao pekee kwenye mchezo huo dakika ya 35 na alitolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 76.
Licha ya ushindi huo, United haitasonga mbele kwenye fainali kwa kuwa ilipoteza mchezo wa kwanza kwa kufungwa mabao 3-0 na kufanya itolewe kwa jumla ya mabao 3-2.
"Guardiola alikuwa anafikiria sana mechi yake na akashindwa kuzuia hisia zake jambo lililomfanya hata ashindwe kupanga kikosi kwa umakini akiwa na wachezaji wake ndani ya Uwanja wa Etihad.
"Jambo hilo liliwapa nafasi United kucheza kwa kujiamini na kufanya makubwa ambayo yaliwapa matokeo na ingekuwa hivyo mpaka mwisho basi habari ingekuwa nyingine," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic