January 28, 2020


TIMU ya Kijitonyama Veterans wikiendi hii ilifanikiwa kupata viongozi wapya watakaoiongoza timu hiyo kwa kipindi cha miaka minne baada ya ya kufanya uchaguzi.
Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Uwanja wa Bora, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti aliyeshinda ni Lupiana Michael Lupiana ‘Rashford, Makamu Mwenyekiti ni Petro Malima ‘Sadio Mane'.
Wakati katibu akiwa ni Amon Petro, Mratibu Majuto Omary, Mwekahazina, Ally Feruzi ‘Teacher’ huku Ofisa Habari akiwa ni Wilbert Molandi ambaye amesema kuwa mpango mkubwa utakuwa ni kuwatumia wachezaji wenye uzoefu kutoa mafunzo ikiwa ni pamoja na Bernard Morrison wa Yanga, Meddie Kagere wa Simba na Juma Kaseja wa KMC.
Pamoja na viongozi wa kuchaguliwa, wajumbe wanne waliteuliwa kuunda Kamati ya Utendaji ambao ni Talib Chuji, John Mbitu ‘Morata’, Hamza Nzowa na Khalid Kahatano ‘Messi’.
Akizungumzia uchaguzi huo, Ofisa Habari wa timu hiyo, Wilbert Molandi amesema kuwa:- "Baada ya uchaguzi huo, sasa hivi viongozi wote tunaelekeza nguvu zetu katika kuifanya timu yetu kuwa bora na yenye mafanikio na kikubwa kufikia malengo tuliyokubaliana katika kipindi hichi ambacho viongozi wapya wameingia madarakani.
 "Mipango ni mingi tunahitaji kuona timu inafikia malengo na kutembelewa na wengi wenye uzoefu kwa ajili ya kutoa somo kwa wachezaji, imani ni kubwa na kazi tutafanya kikubwa mashabiki waendelee kutupa sapoti,".

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic