January 30, 2020


KOCHA Mkuu wa Aston Villa, Dean Smith amesema kuwa alijua kwamba lazima nguvu ya Mbwana Samatta ingefika ukingoni dakika ya 60-65.

Samatta ameanza maisha mapya ndani ya timu ya Aston Villa baada ya kusaini dili la miaka minne na nusu akitokea Klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji.

Mchezo wake wa kwanza ulikuwa dhidi ya Leicester City ambao ulikuwa ni nusu fainali ya Kombe la Carabao na Mtanzania huyo alicheza dakika 65 kwenye mechi yake ya kwanza na timu yake ilishinda mabao 2-1.

 "Nilijua kwamba angechoka kati ya dakika 60-65 kutokana na kutokuwa na timu kwa muda mrefu ila amefanya vizuri anakuja taratibu.

"Ule mpira ambao alikosana nao ulipaswa umpe wepesi kwenye miguu yake kama angefunga ila kwa kuwa ameshindwa kufunga sio mbaya ni mwanzo mzuri kwake," amesema.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic