January 30, 2020


BAADA ya mshambuliaji wa JS Saoura, Thomas Ulimwengu kupata dili la kurejea kwenye Klabu yake ya zamani ya TP Mazembe, Saleh Jembe ametuma ujumbe huu wa wazi kwake namna hii:-

Thomas Ulimwengu umekuwa ukipambana sana lakini wengi wamekuwa wakikukatisha tamaa sana wakati hawajui safari yako ina mwendo na masahibu yapi.

Lawama, lawama, lawama na maneno ya chuki yanayoashiria ufahamu wenye lawama uliojaa chuki.

Kitu kizuri unaelewa na unajua unachohitaji, ndoto zako ni kwa ajili ya maisha yako. Wengi wanaolaumu hatujui wanataka nini na wamefanya nini katika ndoto zao na hujawahi kuwalaumu.

Endelea kusonga, TP Mazembe bado ni kubwa sana, kukusajili maana yake bado wanatambua uwezo wako.

Na Watanzania walipaswa kujivunia zaidi kuwa wewe mmoja wa wachezaji wa Kitanzania waliothubutu na kupata nafasi ya kucheza katika nchi za Afrika kama DRC, Sudan na Algeria ambazo zote ni bora kisoka kuliko Tanzania.

Mimi NAKUPA moyo, kurudi Mazembe si KUFELI badala yake ni mwendelezo wa safari ya maisha yako kisoka na Mungu ndiye anayejua mwisho wake... Umejitajidi sana, bila kupita Simba, Yanga wala Azam na leo ni mchezaji unayefahamika Afrika ukiwa na rekodi kibao.

4 COMMENTS:

  1. Mungu atakusaidia utafika malengo yako

    ReplyDelete
  2. Angerudi Simba tu kuipigania klabu ya Nyumbani Africa, angepumzika roho yake,angefanya kazi kwa utulivu na mazali ni mtu mwenye melengo asingefeli na pengine ni rahisi kutoka na kuingia Simba kuliko Mazembe. Deo Kanda,shibob,chama ni kaaliba ya wachezaji amabao angefanya kazi nao vizuri. Unajua bado tuna kasumba kuwa Simba au Azam ni timu za kawaida lakini kiukweli zinawachezaji muhimu au roho za timu za Taifa kwa mataifa ambayo yametuzidi kimpira .

    ReplyDelete
  3. You are obsolutly speaking truth my brother above there,ukiondoa ushabiki wa usimba,uazam,uyanga na unamungo,AZAM,SIMBA ni miongoni mwa timu zenye wachezaji wakubwa sana tena wenye heshima mno kwenye nchi zao isipokua tatizo lipo kwa watanzania,wengi wetu hatujui na wala hatuna matarajio yakujua umuhimu na thaman ya wachezaji hawa ndani ya klabu na hata wakiwa na timu zao za TAIFA,hii inatokana na ufinyu wa kutokujua mambo yanayohusiana na soka,inapaswa itolewe elimu kwakutumia mbinu maalumu,labda inawezekana tukawa na mtazamo mkubwa kidogo,unajua hii ishu ya wachezaji wa kimataifa sio ya mchezo,sasaivi wengi wanasoma mazingira kwamba mashabiki wanataka nini uwanjani bila yakuzingatia timu au klabu ipo katika hali gani na ninapswa kufanya nini ambacho ndicho haswa kilichonileta hapa,MARISON ameshawasoma mashabiki wa yanga na ameona wanapenda jambo fulani,sasa angalia klabu ya yanga inataka nini currently alafu badala yakufanya kilichokuleta unaleta mbwembwe ambazo maranying sana inakuaga kama ziada baada yakua umetimiza majukumu yako ipasavyo,mbona akina chama,shibobo,kanda hawafanyi mbwembwe?hapa ndio utakapojifunza kwamba simba inaangalia watu wa kazi kwa maslahi ya klabu na sio kufurahisha mashabiki nakusahau majukumu,nipo hapa nasubiria povu lenu.

    ReplyDelete
  4. Ila tusishangae sana maana hata ukiangalia chanzo na asili ya simba(zaman sandalend) ni ufinyu wa elimu na uongozi mbovu uliokuwepo kipindi cha upamoja,na hapo ndipo wasomi wachache walipoamua kuliamsha dude na kuchukua wachezaji wao nakuiasisi klabu yetu pendwa ya simba ambapo mpaka kesho ndio klabu pekee ndani ya afrika mashariki inayoongozwa kisomi zaidi tena na wasomi,mungu ibariki simba kwa hilo,mpaka sasa ile laana ya wazee waliokua na mchango mkubwa katika kuendesha klabu kisomi nikimaanisha yanga bado inawatesa ndiomana ni ngumu sana muwekezaji kuingia mkataba na yanga kwasababu ya hao wazee ambao wana mitazamo yakizamani iliyopingwa na wasomi wachache walioamua kunitenga baada yakukataliwa mapendekezo yao katika mfumo wa uendeshaji wa klabu.narudia tena povu ruksaaaaaaaa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic