January 26, 2020


SVEN Vanndrbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kuna tatizo kubwa la mawasiliano kwa wachezaji wake jambo ambalo linawafanya washindwe kupata mabao mengi wakiwa ndani ya Uwanja.

Simba, Jana, Januari 25 iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Mwadui kwenye mchezo wa hatua ya 32 ya Kombe la Shirikisho na kuipa nafasi ya kusonga mbele hatua ya 16 bora.

Mabao ya Simba yalifungwa na Clatosu Chama na lile la ushindi likifungwa na Francis Kahata huku bao pekee la Mwadui likifungwa na Gerald Mdamu.
Akizungumza na Saleh Jembe, Sven amesema kuwa walikuwa na nafasi ya kushinda kwa mabao mengi wachezaji wake walishindwa kutumia nafasi ambazo walizipata ndani ya kumi na nane.

"Tulikuwa na uwezo wa kufunga mabao mengi ila wachezaji wangu walishindwa kuwa na mawasiliano mazuri ndani ya uwanja jambo ambalo limewafanya wavune ushindi mwembamba kwenye mchezo wetu ambao tulistahili kufunga mabao mengi zaidi ya haya mawili tuliyopata," amesema.

4 COMMENTS:

  1. KOCHA anazungumzia mawasiliano baina ya wachezaji nä kanjanja anatafsiri tatizo ni lugha.

    ReplyDelete
  2. Sijaelewa kufunga maagoli na mawasiliano inakaaje hapo.

    ReplyDelete
  3. MIMI NINACHOJUA MPIRA UNA KUGHA YAKE HPO NDIPO PENYE TATZO

    ReplyDelete
  4. Mi nafikiri mawasiliano yes yanaweza kufanya Simba ikakosa magoli, nimemuelewa sio mawasiliano ya kuongea ila kwa kawaida washambuliaji mikimbio yao inatakiwa iwe na mawasiliano kwamba mi nikienda kulia wewe nenda kushoto, nikishika mpira tafuta open space nikupasie au mpira ukienda pembeni subiri krosi au V pasi ndani ya box, nilicho kiona simba forward zao zina mikimbio isiyo na faida, mtu kama Kagere yeye ni straika wa mwisho lakini kuna wakati humuoni ndani ya 18 na pia huoni nani wa kumsaidia hasa zikipatikana rebounce... Ni mambo madogo madogo tu yanaleta shida. Chama anatumika kama second strika lakini yule ni midfielder kamili ndio maana kuna wakti timu ikishambulia humuoni pale mbele anaweza kuwa chini namba 8 au pepmbeni badala ya kucheza kama namba 9. Kuna maana ya kumuanzisha Boko na Kagere halafu Chama na Dilunga wakawa Winger Midifielder..attacking midfielder namba 8 akakaa Shiboub/Ajibu na Defending midfielder akawa Mkude/Ndemla...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic