January 26, 2020


BERNARD Morrison, kiungo mpya wa Yanga amesema kuwa mashabiki wasiwe na hofu naye ataongeza mkataba mwingine mrefu ili kuendelea kuwapa burudani.

Inaelezwa kuwa, Morrison alipewa kandarasi ya miezi sita inayotoa nafasi kwa wapinzani watani wa jadi wao Simba kufanya mazungumzo naye endapo watamhitaji.

 Kiungo huyo raia wa Ghana amesema hawezi kuwaangusha mashabiki na uongozi wa Yanga kuhusu suala la mkataba wake.

"Nimesaini ndani ya Yana na tayari nimeanza kuzoeana na wachezaji hivyo suala la kusepa kwa sasa halipo na nitazungumza na uongozi ili kujua tunafikia hatua gani hatuwezi kushindwana,".

Imeelezwa kuwa tayari uongozi wa Yanga umefanya naye mazungumzo kwa ajili ya kumpa mkataba mrefu utakaomzuia kufanya mazungumzo na timu nyingine.

2 COMMENTS:

  1. Aisee kiukweli jamaa huyu ni shida hasa blog yake nimefatilia habari za Humu ndani mpaka kero ni marrison tuuuuu mara niyonzima halafu habar ni zile zile sioni kipya hata kidogo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic