January 29, 2020

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa timu ya Namungo amesema kuwa leo ataingia na mbinu mpya itakayompa nguvu ya kupata pointi tatu kwenye mchezo wao utakaochezwa Uwanja wa Taifa, saa 1:00 Usiku.
Namungo iliyo nafasi ya tano kwenye msimamo ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 16 itamenyana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 41 baada ya kucheza mechi 16.
Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa moja ya mpango mkubwa wa timu yake ni kupata pointi tatu mbele ya Simba ili kuwajengea wachezaji wake hali ya kujiamini.
“Mchezo wetu utakuwa mgumu na wenye ushindani, unapocheza na bingwa lazima uwe na tahadhari kabla hajakuumiza tunalitambua hilo na tutaingia uwanjani kwa tahadhari tukiwa na malengo ya kuzipata pointi tatu muhimu mashabiki watupe sapoti,"amesema.

Mechi iliyopita Namungo ilishinda mabao 3-2 mbele ya Prisons Uwanja wa Samora huku Simba ikishinda mabao 4-1 mbele ya Alliance Uwanja wa CCM Kirumba.

2 COMMENTS:

  1. Mnazipata mbona,kikubwa imani na dua.wana wenge la KABWILI mkikaza mnachukua leo maana janja imeshajulikana sasa.

    ReplyDelete
  2. Na kwa maneno yao ya kwamba wao tayari ni mabingwa wa ligi kuu ambao watacheza klabu bingwa inazidi kuwafunga na kutuoa taswira kwamba inawezekana kuna ukweli simba hua ananunua mechi nakupanga matokeo kabla ya mechi,kwa maana kwa wale wakuweka mpunga mezani hapa mkeka hauwezi kuchanika.mwaka huu kombe linarudi yanga au azam maana janja janja imeshajulikana.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic